Akizungumza
kwenye ziara yake mjini Geita ya kuzindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya
madarasa na zahanati Mhandisi Luhumbi amepokea malalamiko ya wakazi wa
Machinjioni waliodai kutosomewa taarifa za mapato na matumizi ya fedha zao.
Mhandisi
Luhumbi alisema kuwa endapo kama itakabainika
kuwa kiongozi wa mtaa, kijiji au Kata ametumia vibaya fedha za wananchi
anapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria na kuzirejesha fedha hizo.
“Mkurugenzi leta timu ya ukaguzi wa hesabu za
Serikali ili ikague na kujiridhisha kama kuna fedha yoyote iliyochukuliwa
pasipo maelezo yanayojitosheleza hatua zichukuliwe haraka kwa wote
watakaobainika kuhusika". Alisisitiza
Luhumbi.
Mheshimiwa
Robert ameongeza kuwa ukaguzi huo ufanyike kuanzia mwaka 2014 hadi 2017 kisha
apate taarifa hiyo ofisini. Akiwa katika
Halmashauri hiyo Mkuu wa Mkoa amepongeza jitihada zinazofanywa na wananchi za
kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo licha ya kuwepo
changamoto nyingi katika maeneo yao.
Diwani wa
Kata ya Mgusu Bw Pastory Ruhusa amemueleza Mkuu wa Mkoa changamoto
wanazokumbana nazo kutokana na kukosekana kwa kituo cha afya kuwa ni pamoja na
wakina mama kujifungulia njiani na muda mwingine watu wengi wamejikuta
wakipoteza maisha kutokana na kukosekana kwa zahanati kwenye kata hiyo.
“Mkuu hapa
tumezungukwa na mgodi na ulituhaidi kutuchangia sh,milioni mia moj lakini
tunaona kama ni maneno tu kwani sasa imepita miaka miwili mgodi haujatekeleza
hiyo ahadi kiukweli tunapata shida sana kutokana na kwamba kata yetu ni mpya na
uhitaji ni mkubwa sanaa tunaomba msaada wako”Alisema Ruhusa.
Mkuu wa Mkoa
amehitimisha ziara yake ya Mkoa mzima katika Halmashauri ya Mji Geita kwa
kutembelea na kushirikiana na wananchi kujenga nyumba pacha ya walimu (Two in
one) Shule ya Msingi Shinamwendwa, ujenzi wa kituo cha Zahanati Mtaa wa Nyakato
, ujenzi wa vyumba vya madarasa viwili, ujenzi wa jengo la utawala shule ya
Sekondari Mgusu pamoja na kukagua eneo la kujenga Zahanati katika Kata hiyo. Katika ziara hiyo ya Mkoa mzima Mheshimiwa
Gabriel amefanikiwa kutembelea Wilaya zote tano (5) na Halmashauri sita(6) na
kufanikiwa kujenga, kutembelea na kuanzisha jumla ya miradi 19 katika Sekta za
Afya, Maji na Ujenzi huku akikusanya zaidi ya mifuko 800 ya Saruji, tofali za
Block 500, Mbao 50. Haya yote ni matokeo ya kazi aliyoianza ya kushirikiana na
wananchi kutekeleza miradi ya maendeleo katika kila kijiji ndani ya Mkoa huu
lengo kuu likiwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora karibu na maeneo yao
pia kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa na Zahanati Mkoa humu.
Wananchi
wote katika maeneo aliyopita kufanya kazi wameonyesha kuridhishwa na utendaji
kazi wa Serikali na kuamua kuunga mkono juhudi hizi kwa kushiriki katika
utekelezaji wa miradi kama vile kusoma maji, kubeba mawe, mchanga, kokoto,
kuchimba misingi na vijana kujitolea kujenga miradi hii.
0 comments:
Post a Comment