Home » » DHAHABU ZA MIL 700 ZAKAMATWA ZIKISAFIRISHWA KWA MAGENDO.

DHAHABU ZA MIL 700 ZAKAMATWA ZIKISAFIRISHWA KWA MAGENDO.


Jumla ya Gramu 3263.72 za dhahabu zenye thamamani ya

 shilingi milioni 749,509,531.94 zimekamatwa zikisafirishwa kinyume cha sheria mkoani Geita.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linawashikilia watu watatu 

waliokamatwa wakiwa na dhahabu hizo wakisafirisha kwa

 njia za magendo pia kinyume cha sheria kwa kutumia gari 

aina ya Toyota Premio yenye namba za usajili T.739 EEH mali ya

 Emanuel Kidenya Mkazi wa Kahama, Shinyanga.

Waliokamatwa ni Yohana Idama (34), Mkazi ya Nyamhongolo 

wilaya ya Ilemela Mwanza, Moshi Manzili (26), Mkazi wa Bariadi

 Simiyu na Hamidu Salum (25), Mkazi wa Nyasubi wilaya ya Kahama Shinyanga.

Watuhumiwa hao wamekamatwa Machi 24, 2025 majira ya

 saa 5 usiku katika Mtaa wa Kapera Wilayani Bukombe baada 

ya Jeshi la Polisi kupata taarifa za siri na kuweka mtego 

uliofanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hawa. Baada

 ya upekuzi wa gari kufanyika, walikutwa wakiwa na kiasi

 hicho cha dhahabu kilichokuwa kimefichwa ndani ya gari hiyo.

Uchunguzi wa tukio hili kwa kushirikiana na Mamlaka 

nyingine unaendelea kufanyika sambamba na kubaini 

na kuwakamata watakaobainika kujihusisha na uhalifu huo

 na kuwafikisha Mahakamani mara moja.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuacha mara 

moja kujihusisha na vitendo vya magendo na biashara 

haramu kwani halitasita kuchukua hatua kali za kisheria

 kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo. 


0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa