JAMII ya
wafugaji kabila la Wahima mkoani Geita wameiomba Serikali kuwadhibiti baadhi ya
watendaji wa vijiji, kata na maofisa uhamiaji ambao wamekuwa wakiwaomba
rushwa ya Fedha na Mifugo ili wasitajwe kwenye oporosheni ya kuwaondoa
wahamiaji haramu.
Hatua hiyo ni kufuatia kuwafananisha Wahima Raia
wa Tanzania na Wahamiaji Haramu jamii ya Wanyarwanda hali ambayo wamedai kuwa
ni unyanyasaji wa Kijinsia na ukiukwaji wa haki za Binadamu.
Wakizungumza na Kituo hiki wananchi hao wamesema
baadhi ya watendaji wa vijiji,kata na maofisa uhamiaji mkoani hapa wameanzisha
mkakati wa kukusanya fedha kwa njia ya rushwa wakitishia kuwakamata watu ambao
wanafanana kwa sura na kabila la Wanyarwanda.
Mmoja wa Wawahima, Sospeter Karoli akizungumzia
historia ya kabla hilo amesema wao ni raia halali wa Tanzania Tangu miaka ya
1675 ambapo mababu zao walipoingia nchini wakitokea Ethiopia Kupitia mjini
Bunyoro nchini Uganda na baadaye kutawala eneo la Karagwe mkoani Kagera.
Akizungumzia Tuhuma za baadhi ya maofisa
uhamiaji na watendaji wa kata na vijiji za kuomba Rushwa Kamanda wa Uhamiaji
mkoa wa Geita Charles Washima amekiri kupata taarifa hizo hasa katika wilaya ya
Bukombe na hivyo kuahidi kuwafuatilia viongozi hao ili kuwachukulia hatua za
kisheria.
Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya
kawaida,Mzee Lumenangabo Kichukuma(100)Mhima mkazi wa Bugulula wilayani
Geita ametishia kujiua kwa kujinyonga ama kujizamisha majini endapo serikali
itamkamata kumpeleka katika nchi ambayo hakuzaliwa ili hali yeye akidai kuwa ni
Raia halali wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment