Home » » Madiwani Geita wagombea mapato ya dhahabu GGM

Madiwani Geita wagombea mapato ya dhahabu GGM

KIKAO cha baraza la madiwani wa halmashauri ya mji na wilaya ya Geita cha kujadili mapendekezo juu ya mgawanyo wa mapato yatokanayo na shughuli za uchimbaji wa dhahabu katika mgodi wa Geita (GGM) Jana kiliingia dosari baada ya madiwani wa Halmashauri ya mji kususia kikao hicho.

Madiwani hao walisusia kikao hicho baada ya kutoka nje wakipinga maamuzi ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Geita, Elisha Lupuga kupitisha taarifa ya mgawo wa mapato hayo ambayo walidai maamuzi yake hayakuwa sahihi.
Hatua hiyo ilikuja muda mfupi baada ya kuibuka mvutano uliodumu kwa muda wa saa moja wakati wa kujadili taarifa hiyo ya mapato yatokanayo na Kampuni ya GGM.
Akitoa Maamuzi hayo mwenyekiti Lupuga amesema anakubaliana na taarifa ya tume hiyo kwa kupendekeza halmashauri ya mji kuchukua asilimia 56 na halmashauri ya wilaya ya Geita kuchukua asilimia 44 ya mapato yanayotolewa na mgodi huo.
Maamuzi hayo yalisababisha madai hao kususia kikao hicho kwa madai kwamba taarifa ya tume hiyo haikuwa sihihi kutokana na wajumbe wa tume hiyo kutoka halmashauri ya mji kutoshirikishwa katika maandalizi yake.
Akizungumzia hatua hiyo mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Geita, Martine Kwilasa amesema wao walipendekeza kwamba, almashauri ya mji kupewa asilimia 70 na halmashauri ya wilaya ipewe asilimia 30 kutokana na eneo kubwa na mgodi wa Geita kuwa kwenye halmashauri ya Mji.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa