Home » » Diwani wa Kasamwa atakiwa kutolipa kisasi

Diwani wa Kasamwa atakiwa kutolipa kisasi




na John Sanjo, Geita


MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kanda ya Ziwa Magharibi, Peter Makele, amemtaka Diwani wa Kasamwa, Fabian Mahenge, kutolipa kisasi kwa waliomsababishia kufungwa akitetea masilahi ya Wana Kasamwa.

Kauli ya mwenyekiti huyo ilikuja jana baada ya Mahenge kumaliza adhabu ya kifungo cha miezi mitatu kabla ya rufaa yake kukubaliwa, ambapo diwani huyo na wenzake watano walifungwa.

Pamoja na diwani huyo, wengine waliotumikia kifungo hicho kwa makosa ya uchochezi na kusababisha nyumba ya mganga wa kienyeji kuchomwa moto ni Yombo Petro, Zenze Richard, Nomelo Ndikusataga, Nicholaus Buseng'hwa na Ngiyu Lung’wecha.

Ilidaiwa kwamba mganga huyo alikaidi agizo la kupisha ujenzi wa kituo cha mabasi mjini Geita.
Kwa upande wake Mahenge alisema hatarudi nyuma katika kupigania masilahi ya wakazi wa kata hiyo huku akisisitiza kwamba atafanya hivyo kwa mujibu wa sheria bila woga.

CHANZO: DAIMA

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa