SH10, 000 YAWAPONZA MUUGUZI, MHUDUMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Geita imewaburuta mahakamani watumishi wawili wa Hospitali ya Wilaya ya Bukombe wakikabiliwa na mashtaka mawili tofauti likiwemo la kuomba na kupokea rushwa ya Sh10,000.
Walioburuzwa mahakamani ni Elizabeth Emanuel ambaye ni muuguzi na David Zakayo ambaye ni mhudumu wa afya katika hospitali hiyo.
Mwendesha mashtaka wa Takukuru mkoani geita, Kelvin Murusuri ameieleza mahakama kuwa washtakiwa wote kwa pamoja waliomba na kupokea rushwa ya Sh10, 000.
Wakisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Veronica Selemani, washtakiwa hao wamedaiwa kutendo kosa hilo Julai 13, kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Katika maelezo ya makossa hayo ilielezwa kuwa wakiwa eneo lao la kazi, washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuomba kiasi hicho cha fedha kutoka kwa mgonjwa aliyeelezwa kuwa ni mzee mwenye umri wa miaka 72 ambaye hata hivyo hakutajwa jina.
Fedha hizo zilidaiwa kuwa ni gharama za mzee huyo kupatiwa majibu ya vipimo alivyochukuliwa alipofika hospitalini hapo kwa matibabu.
Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Wazee ya Mwaka 2003, mgonjwa huyo hakutakiwa kulipia gharama za matibabu.
Washitakiwa wamekana mashitaka na kuachiwa kwa dhamana ya hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh4 milioni na wadhamini wawili hadi Agosti 16, shauri hilo litakapokuja kwa ajili ya kusomewa maelezo ya mashtaka baada ya upande wa Jamhuri kueleza kuwa upelelezi umekamilika.

Chanzo Mwananchi

MSUKUMA KUWANIA UENYEKITI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  

Ndoto za mbunge wa jimbo la Geita Joseph Kasheku (msukuma) za kuendelea kuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita zipo mikononi mwa kamati kuu ya Taifa ya chama kutokana na kanuni mpya za chama hicho kutoruhusu kiongozi kuwa na kofia mbili za uongozi.
Msukuma ni miongoni mwa wanachama 13 wa CCM ambao wamejitokeza leo kuchukua fomu za kugombea nafasi za uenyekiti ngazi ya mkoa.
Katibu wa CCM mkoani hapa Adam Ngallawa amesema kwa mujibu wa kanuni mpya ya uchaguzi ndani ya chama ya mwaka 2017 mbunge au diwani hapaswi kuomba nafasi yoyote lakini katika mkoa huo wapo waliojitokeza na hatma yao itatolewa na kamati kuu ya Taifa chini ya mwenyekiti wake Rais John Magufuli.
Amesema mbali na Msukuma pia yupo mwenyekiti wa baraza la madiwani wa halmashauri ya mji wa Geita Leornad Bugomola ambae ni diwani wa kata ya Bombambili ambaye ameomba nafasi ya ujumbe wa halmashauri kuu ya taifa .
Ngallawa amewataja wengine ambao wamechukua a fomu ya kugombea nafasi ya uenyekiti kuwa ni Bujukano John ,Paul Luhangija ,John Luhemeja, Deus Lynkando, Ernest Nyororo na Alhaji Kalidushi ambae kwa sasa ni katibu mwenyezi wa chama hicho.
Wengine ni James Msarika,William Misalaba ,Elias Mayila,George Mapalala,Simon Mayengo na Menge Malago.
Amesema katika nafasi ya katibu siasa na uenezi imeombwa na watu saba ambao ni David Azari,Ibrahim Juma ,Agustino Kabelela ,George Mapalala,Lusenga Manjale ,Thobias Meleka na Donald Rubigisa.
Nafasi za ujumbe wa halmashauri kuu ya Taifa imeombwa na wananchama 13 ambao ni Leornad Bugomola ambae ni diwani,Lyidia Bupilipili ambae ni mkuu wa wilaya ya Bunda,Idd Kassim na Musa Derefa.
Wengine ni Mashauri Kaliango Genes Katabalo ,Deusdedut Katwale ,Paul Luhangija, Sashisha Mafue ,Ruvenatus Malecha ,Mapambano Manyungu ,Mary Mazula na Manumba Stephano
“Ni kweli kanuni za uchaguzi haziruhusu mtu mwenye nafasi nyingine ya kisiasa kama mbunge na diwani kugombea nafasi ya uongozi ndani ya chama hawa walichukua fomu na wenye mamlaka ya maamuzi juu yao ni kamatikuu ya Taifa”amesema Ngallawa
Ngallawa aliwataka wagombea hao kuepuka kutoa takrima yoyote kwa wanachama au kuanza kujieleza kwa wananchi na kwamba wagombea wote watajinadi siku ya uchaguzi ambayo ndio siku ya majina ya walioteuliwa kugombea yatatajwa.

Chanzo Mwananchi

MAOFISA UGANI WA WILAYA YA BUKOMBE WATAKIWA KUWA NA KUMBUKUMBU ZA KILIMO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


 Mkuu wa wilaya ya Bukombe,. Joseph Maganga (kulia), akizungumza na maofisa Ugani wa Wilaya hiyo kwenye mafunzo ya kilimo cha mazao ya Mihogo,Pambana Viazi lishe yaliyoandaliwa na Tume yaTaifa yaSayansi na Teknolojia(COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia OFAB. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa wilaya hiyo, Zacharia Bwile na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Baraka Maganga

Mshauri wa Jukwaa la Masuala ya Bioteknolojia (OFAB) Dk. Nicholaus Nyange, akitoa mada kuhusu matumizi ya Bioteknolojia ya kilimo.

Maofisa Ugani wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa wilaya hiyo, Joseph Machibya akizungumza katika mafunzo hayo.
Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi (kulia), akifuatilia mafunzo hayo. Kutoka kushoto ni Waandishi wa habari zakilimo, Gelard Kitabu na Carvin Gwabara.
Mtafiti wa kilimo kutoka COSTEC, Bestina Daniel akizungumza kwa niaba wa Mkurigenzi Mkuu wa Costech wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Maofisa Ugani wa Wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Wanahabari wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Baraka Maganga akizungumza kwenye mafunzo hayo. 
Mtafiti wa Kilimo kutoka Kituo cha Ukiriguru Mwanza, Bakar Chirimi akitoa mada kwenye mafunzo hayo.
Watafiti wa kilimo na maofisa Ugani wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Joseph Maganga.

WILAYA YA GEITA KUTENGA MILIONI 50 KWA AJILI YA MAFUNZO YA KUBORESHA KILIMO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Mkuu wa Wilaya ya Geita Herman Kapufi akizungumza wakati akifungua  mafunzo ya siku moja kwa maofisa ugani  wa wilayani yake wilayani humo jana yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),  yenye lengo  la kuwakumbusha wataalamu hao wa kilimo nafasi yao pamoja na kuwapatia mbinu mpya za kisasa katika kulima mazao ya Mihogo, Pamba na Viazi vitamu katika kuelekea serikali ya viwanda. 

RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA AKABIDHI NYUMBA 50 ZA WATUMISHI WA AFYA KATIKA MIKOA YA SIMIYU, KAGERA NA GEITA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
MKAPA KUKABIDHI NYUMBA 10 HOSPITALI YA WILAYA YA CHATO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Chato
RAIS mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa amewasili wilayani hapa mkoani Geita ambapo leo anatarajiwa kukabidhi nyumba kumi kwa Hospitali ya Wilaya ya Chato zilizojengwa kwa ufadhili wa Mkapa Foundation.
Mkapa ambaye alikuwa ameambatana na mkewe, Mama Anna Mkapa walipokelewa na mwenyeji wake ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli aliyekuwa sambamba na mkewe, Mama Janeth Magufuli.
Katika msafara huo pia Rais mstaafu Mkapa ameambatana na Balozi wa Japan hapa nchini, Masaharn Yoshida ambaye leo anakabidhi mashine ya kukamulia mafuta ya alizeti kwa chama cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato (AMCOSS). Rais mstaafu, Mkapa anatarajiwa pia leo kuhudhuria mkutano wa hadhara utakaohutubiwa na mwenyeji wake Rais Magufuli utakaofanyika katika Uwanja wa Mazaina ulioko mjini
CHANZO HABARI LEO

PLAN INTERNATIONAL GEITA YAKABIDHI ZAWADI MBALI MBALI KWA WATOTO WALIOFANYA VIZURI UANDISHI WA BARUA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Meneja wa Plan Mkoani Geita,Baraka Mgohamwende akimkabidhi Zawadi moja kati ya mtoto aliyefanya vizuri kwenye mashindano ya kuandika Barua.
Mratibu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Ufadhili Plan Geita ,Imani Mgohamwende akielezea juu ya kuwatambua baadhi ya watoto ambao wamefanya vizuri kwenye mashindano ya uandishi wa barua.

Meneja wa Plan Mkoani Geita,Baraka Mgohamwende  akielezea dhumuni la kutoa zawadi kwa washindi.
Moja Kati ya vijana ambao ameshinda uandishi wa Barua akionesha moja kati ya zawadi ambazo amepatiwa na Plan.


Mzee  Shedrack Mashamba akikabidhiwa Chati cha Pongezi kutokana na kujitolea kwenye maswala ya Plan kwenye kata ya Nyang’uku na  Meneja wa Plan Mkoani Geita,Baraka Mgohamwende .

Mzee Juma Maheka akikabidhiwa chati cha utambuzi na   Meneja wa Plan Mkoani Geita,Baraka Mgohamwende .
Picha na Maduka Online.

UFAHAMU MKOA WA GEITA KWA UPANA ZAIDI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Meja Jenerali (Mst) Ezekiel E. Kyunga
Mkoa huu ulianzishwa mwaka 2012 kutoka  sehemu ya mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Kagera ukiundwa na Wilaya tano zenye Halmashuri Sita na majimbo saba (7) ya Uchaguzi. Mkoa una ukubwa wa eneo la km21,879 linalotumika katika shughuli za Kilimo cha mazao ya (Nanasi, Mahindi, Mpunga, Alizeti, Pamba na mazao mengine), Uchimbaji wa Madini aina ya Dhahabu katika Mgodi Mkubwa wa GGM na migodi midogo midogo, Biashara, Ufugaji, na uvuvi hususan maeneo ya Wilaya za Geita na Chato. Aidha Mkoa huu unasifika kuwa na hifadhi ya misitu mikubwa ya Kigosi /Moyowosi na kisiwa cha Rubondo kilicho ndani ya ziwa Victoria, kisiwa hiki kina wanyama adimu kama Statunga, Sokwe na eneo la mazalia ya samaki aina ya sangara.

Chanzo Tovuti ya Mkoa wa Geita 

UCHELEWESHAJI WA PEMBEJEO UMETAJWA KUPOROMOSHA KILIMO CHA PAMBA WILAYANI MBOGWE MKOANI GEITA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Mbogwe, (kulia), Elias Kayandabila, akizungumza  na waandishi wa habari, walioongozana na wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) pamoja na Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB) waliopo mkoani Geita kwa ziara ya kutoa mafunzo ya kilimo chenye tija kwa maofisa ugani.

MBEGU BORA ZA MHOGO ZINAHITAJIKA KUWANUSURU WAKULIMA WILAYANI CHATO MKOANI GEITA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ipandikilo kilichopo katika Halmshauri ya Wilaya ya Chato, Lazaro Kagundulilo (kulia), akizungumza na wanahabari pamoja na  wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) na , Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB), wilayani humo jana. Wataalamu hao wa kilimo wapo katika wilaya hiyo kwa ziara ya kutoa mafunzo ya kilimo chenye tija kwa maofisa ugani wa Mkoa wa Geita.

CHATO WATAKIWA KUCHANGAMKIA KILIMO CHA MIHOGO CHENYE TIJA ILI KUINGIA KATIKA SOKO LA KIMATAIFA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita (RAS), Selestine Gesimba akizungumza na wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB) pamoja na wanahabari walipofika ofisini kwake wakiwa katika ziara ya kutoa mafunzo ya kilimo chenye tija kwa maofisa ugani wa mkoa huo leo.

(VIDEO) KIJANA PAUL MWILOMBWA MLEMAVU WA VIUNGO ANAOMBA MSAADA WAKO ILI AWEZE KUTIMIZA MALENGO YAKE KUPITIA SHUGHULI ANAYOIFANYA

Paul Ibrahim Mwilombwa ni Kijana anayeishi Mkoa wa Geita Wilaya ya Chato, ni mlemavu wa viungo na mwenye kujishughulisha na maswala ya upigaji picha na mambo ya 'Graphic Design'.  hapa anaelezea historia yake na kuwaomba msaada watanzania ili apate kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.

14 akiwamo Mchina wafukiwa mgodini Geita

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga
WATU 14 akiwemo Mchina, wanahofiwa kufa baada ya kufukiwa katika mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya RZ Union Mining Ltd uliopo Kata ya Nyarugusu mkoani Geita.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga alisema watu hao wamefukiwa chini ya mgodi baada ya mlango wa kuingilia kwenye shimo la mgodi kumeguka udongo na kujiziba.
“Usiku wa kuamkia leo (jana) saa tisa kwenye mgodi huo unaoendeshwa na Wachina, mlango wa kuingilia mgodini mmoja ulimeguka na kujifunga watu 14 wakiwa ndani,” alisema Kyunga.
Kyunga alisema kwa mujibu wa kitabu cha orodha ya watu wanaojiandikisha kuingia mgodini, kuna majina ya Watanzania 12 na Mchina.
Aidha, alisema mbali na watu hao 13, pia kuna Mtanzania mmoja ambaye aliingia bila kujiandikisha na hiyo ni kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo hivyo kufanya idadi ya watu waliofukiwa kuwa 14. Kyunga alisema tangu jana asubuhi jitihada mbalimbali za kuondoa udongo kuwaokoa watu hao zinaendelea wakitumia mitambo na wataalamu.
“Kwa kusaidiana na Kampuni ya Geita Gold Mine (GGM) na wataalamu wengine, jitihada zinaendelea ili kuhakikisha tunawaokoa watu hao,” alisema Kyunga. Alisema wakati huo huo wamefanikiwa kutoboa eneo jingine na kupitisha mabomba ya hewa ya oksijeni ili kuwafanya watu hao wasikose hewa.
Chanzo Gazeti la Habari leo

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA PROF. IBRAHIM GAMBARI MJUMBE MAALUM WA RAIS WA NIGERIA, CHATO MKOANI GEITA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
PICHA NA IKULU


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 10 Januari, 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Rais wa Nigeria Profesa Ibrahim Gambari nyumbani kwake Chato Mkoani Geita. Mazungumzo yao yalilenga masuala mbalimbali ya uhusiano kati ya Tanzania na Nigeria.
Rais Magufuli amempongeza Rais Muhammadu Buhari kwa jitihada kubwa anazochukua kwa ajili ya kuleta maendeleo nchini mwaka.
Pia, Rais Magufuli amempongeza Rais Buhari kwa jitihada anazozifanya za kukabiliana na kundi la Boko haramu ili kuhakikisha amani inaendelea kudumu nchini mwake.
Kwa upande wake Mjumbe Maalum wa Rais wa Nigeria, Profesa Ibrahim Gambari amempongeza Rais Magufuli kwa ushindi alioupata na jitihada anazochukua katika kupambana na rushwa na kubana matumizi jambo ambalo linaungwa mkono na wananchi wengi wa Nigeria.
Profesa Gambari alimkabidhi Rais Magufuli barua yenye ujumbe maalum kutoka kwa Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria.


Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato, Geita
10 Januari, 2017

 

Rais Dkt. Magufuli awasalimia wakazi wa Chato Mjini, pia atembelea Shule ya Msingi aliyosoma Chato

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 PICHA NA IKULU

WATU 7 WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA GARI GEITA SIKU YA MKESHA WA KRISMASI WAZIKWA

Mkuu wa wilaya ya Kahama bw. Fadhili nkulu amewaongoza mamia ya wakazi wa wilaya ya Kahama na viunga vyake katika mazishi ya watu saba waliofariki katika ajali ya gari tarehe 24 mwezi huu katika eneo la Kanegere wilayani Mbogwe mkoani Geita akiwemo Padri wa kanisa katoliki la Mt.Karoli Lwanga mjini Kahama muda mfupi kabla ya mkesha wa sikukuu ya Krismasi kuanza.

Akizungumza katika ibada hiyo iliyoongozwa na askofu Flavian Kasala wa jimbo kuu Katoliki Geita na hudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, dini, siasa na waumini wa madhehebu tofauti ya dini mkuu wa wilaya ya Kahama Bw.Fadhili Nkulu amesema msiba huo umeacha pengo kubwa kwa wana Kahama kwani wamempoteza kiongozi shupavu wa kiroho na vijana ambao walikuwa ni tegemeo licha ya kuwa bado walikua wanafunzi huku akiwataka wasihusishe na imani tofauti zisizostahili.

Naye askofu Liberatus Sangu wa kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga amewaasa waumini wa dini zoye kukumbuka kutubu na kuishi maisha ya kumuamini mwenyezi mungu huku Askofu Lidorvic minde wa kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Karoli Lwanga Kahama ambako ndiko mazishi yalikofanyika akitoa neno la faraja kwa waombolezaji.

Nao baadhi ya waombolezaji na wau waliohudhuria katika mazishi hayo wameonyesha masikitiko yao na kuzungumzia msiba huo ambao umeonyesha kuwagusa kwa namna moja au nyingine
CHANZO MICHUZI MEDIA GROUP
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa