Home » » Police day yafana Geita

Police day yafana Geita

JESHI la Polisi nchini limetakiwa kuitumia fursa ya siku ya Polisi kufanya mabadiliko ya kujitambua kuwa ni sehemu ya Jamii kwa kushiriki  katika shughuli za kijamii na kujikumbusha wajibu na majukumu yake katika utendaji wake.

Ili kurejesha imani kwa jamii limetakiwa kujenga mahusiano na jamii hatua ambayo italetaza mafanikio katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu kupitia falsafa ya polisi jamii shirikishi.

Wito huo umetolewa juzi na Mkuu wa mkoa wa Geita Magalula Said  Magalula aliyekuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha Siku ya Polisi Nchini Police day iliyofanyika Kitaifa mkoani Geita mara baada ya kupokea maandamano ya Askari wa vitengo vyote.

Kilele hicho cha siku ya Polisi Nchini kimefanyika jana kitaifa mkoani Geita kama sehemu ya kutoa hamasa kwa wakazi wa mkoa huo kuongeza mchango wao katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu kwa kusogeza sherehe hizo mikoani waliko walengwa nawadau wengi.

Katika kilele hicho Askari polisi wakiongozwa na Kamanda wa polisi wa mkoa wa Geita Leonard Paul walifanya usafi wa mazingira kwenye hospitali ya wilaya ya  Geita na kuishia katika Bwalo la Polisi ambaye alidai kuwa wanafanya hivyo kuashiria kuwa wao ni sehemuya jamii tofati na ukiritimba wa polisi wa kikoloni.

Naibu Kamishna wa Polisi Bwana Michael Kamhanda aliyekuwa maemwakilisha Inpskta jenarali wa polisi Said Mwema alisema kuwa hatua ya kuleta kilele hicho kitaifa kufanyika mkoani Geita nikuonyesha jinsi jehi hilo linavyoutambua mchango wa jamii huko waliko mikoani.

Hata hivyo kilele cha sherehe ya maadhimisho ya siku hiyo hayakufana kwakiasi kikubwa  kutokana na jamii  kutokuwa na utamaduni wa kuchangamana na Askari polisi kutokana na kuwaona kama wao siyo sehemu ya jamii.

Hatua hiyo hatua ikamsukuma mgenirasmi Magalula Said Magalula Mkuu wa mkoa wa Geita kukiri kuwa haikufana na kushauri mwaka ujaotena maadhimisho hayokurejewa kufanyika mkoaniGeita Kitaifa.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa