Geita
HATIMAYE
serikali imekamilisha zoezi la upimaji wa viwanja 18 kwenye eneo lenye ukubwa
wa Hekta 373.6 katika vijiji vya Isamilo na Nyamikoma wilayani Geita
lililotengwa na wizara ya nishati na madini kwa ajili ya wachimbaji wadogo.
Hatua
hiyo ni kutokana malalamiko ya muda mrefu ya wachimbaji wadogo kukosa maeneo
mazuri ya kuchimba kufuatia baadhi ya wenye leseni kuuza leseni zao kwa
wakezaji wakubwa na hivyo kujikuta hawana maeneo mazuri ya kuchimba.
Mkuu
wa mkoa wa Geita Said Magalula amesema hayo jana(Jumatatu) alipokutana na
waandishi wa habari ofisi kwake ili kuzungumzia sekta hiyo ya madini
inayotegemewa na idadi kubwa ya wakazi wa wilaya ya Geita.
Amesema
zoezi la upimaji wa viwanja hivyo vilivyochukua ukubwa wa Hekta 83.45 kati ya
hekta 373.6 limefanyika baada ya kufanyiwa uchunguzi na watalaamu mbalimbali wa
miamba kupitia wakala wa JiolojiaTanzania(GST) na kubaini kuwa eneo hilo lina
miamba yenye madini ya dhahabu.
Kufuatia
kukamilika kwa zoezi hilo mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wananchi wa Geita
kutumia fursa hiyo kutuma maombi ya leseni kwa ofisa madini mkazi kupitia
vikundi vyao vya ushirika(SACCOS) na Vijiji na kwamba hakuna leseni
itakayotolewa kwa mchimbaji mmjo mmoja.
0 comments:
Post a Comment