Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
|
Baiskeli ambazo zimetolewa kwa wawakilishi wa kujitolea kwenye jamii na shirika lisilo la kiserikali la plan international mkoani Geita. |
|
Kushoto ni meneja wa Plan Mkoani Geita, Bw Marcel Madubi na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi wakizungumza wakati wa zoezi la utoaji wa baiskeli. |
|
Meneja wa Plan Mkoani Geita, Bw Marcel Madubi akizungumzia malengo ambayo yamepelekea wao kutoa Baiskeli hizo kwa wawakilishi wa jamii. |
|
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akizungumza na wanufaika wa Baiskeli hizo. |
|
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiendasha Baiskeli ambazo zimekabidhiwa kwa wawakilishi wa jamii. |
|
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akimkabidhi Baiskeli Bi,Lucy John(Katikakati)pembeni kutoka kulia ni Mejena wa Plan ,Bw Marcel Madubi. |
|
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akimkabidhi Baiskeli,Mzee Geofray Kilomba na pembeni ambaye anapiga makofi ni,meneja wa plan Bw,Marcel Madubi.(PICHA NA JOEL MADUKA) |
|
|
|
NA ,CONSOLATA EVARIST GEITA
Shirika
lisilo la kiserikali la Plan International
ambalo linashugulikia masuala ya kulinda na kutetea haki za watoto hususani wa kike
limekabidhi Baiskeli kwa wawakilishi wa kujitolea kwa jamii kwaajiri ya kurahisisha kuwafikia walengwa na kutoa elimu dhidi ya ulinzi wa mtoto.
Akizungumza
wakati wa zoezi la kutoa baiskeli 191
zenye gharama ya shilingi milioni 39,Meneja wa plan Mkoani Geita,Bw Marcel
Madubi alisema kuwa watoto wangi
wamekuwa wakikumbwa na matatizo mengi likiwemo swala la mimba za
utotoni na kuhozwa mapema kitu ambacho
kinaweza kukatisha ndoto zao za kimasomo.
“Wawakilishi
wamekua ni kiungo kibwa kati yao na jamii katika kutafuta takwimu sahihi za
watoto na kuwatafutia ufadhili na tangu plan ifike Geita kume kua na msaada
wakuwatoa watoto kwenye utumikishwaji wa kazi zisizo sahihi mfano kwenye maeneo ya migodi tumeweza
kusaidia kwa kiasi kikubwa”Alisema Madubi.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Geita Herman
kapufi ambae alikua mgeni rasimi katika hafra hiyo alisema msingi wowote wa
maendeleo unaanzia na mtoto kwahiyo ili Taifa liende mbele nilazima watoto waangaliwe kwa umakini
na kwamba chombo ambacho wamepatiwa wawakilishi kitawasaidia kwa kiasi kikubwa
kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Bi,Scholastika
Vitus ambaye ni mmoja kati ya wanafaika wa usafiri huo, alisema kunachangamoto
nyingi zinawakumba watoto kama ukosefu wa mabweni hali ambayo inapelekea wengi
wao kujikuta wakiingia kwenye mahusiano na waendesha boda boda ili mradi waweze
kupata usafiri na kwamba endapo serikali itatilia maanani ujenzi wa mabweni
itakuwa imemsaida mtoto wa kike kuepukana na vishawishi.
0 comments:
Post a Comment