Home » » KAMPUNI YA BLUE COAST INVESTMENT YACHANGIA MADAWATI 200

KAMPUNI YA BLUE COAST INVESTMENT YACHANGIA MADAWATI 200

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Madawati mia mbili ambayo yametolewa na kampuni ya Blue coast Investment iliyopo Mkoani Geita kwa lengo la kusaidia mahitaji ya elimu.

Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akimshukuru mkurugenzi wa kampuni ya Blue coast Investment ,Bw Athanas Inyasi  ambaye yupo katika kwa kujitolea yeye na kampuni yake kutoa madawati kwenye halmashauri ya mji na wa kushoto ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita,Leornad Kiganga Bugomola.

mkurugenzi wa kampuni ya Blue coast Investment ,Bw Athanas Inyasi akimkabidhi mkuu wa Wilaya madawati mia mbili ambayo ameyatoa.

Mkuu wa Wilaya ya Geita.,Mwl Herman Kapufi akipokea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita,wakati wa zoezi la kukabidhiwa madawati mia mbili.(PICHA NA JOEL MADUKA)

Na,Faudhia Sharif ,Geita



Mkurugenzi wa kampuni ya Blue coast Investment Bw Athanas Inyasi amekabidhi madawati 200 yenye thamani ya Sh milioni 15 ili kusaidia shule zenye upungufu wa madawati mkoani Geita.

Akikabidhi madawati hayo mbele ya mkuu wa wilaya ya Geita, Mwl Herman Kapufi, Bw Inyasi alisema akiwa mmoja wa wazazi anapenda kuona wanafunzi wakisoma katika mazingira mazuri ili wafikie ndoto za maisha yao ameguswa na kuamua kutoa madawati hayo na kwamba  wao kama kampuni inayotambua umuhimu wa elimu wataaendelea kushiriki kuchangia vitu mbali mbali katika kuinua elimu.

Akipokea mdawati hayo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi, Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi amempongeza Bw Inyasi kwa jitihada anazozifanya katika kuinua sekta ya elimu mkoani Geita.

Naye Mkurugenzi wa mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinaly alisema kuwa madawati hayo yatasaidia kwani kwa sasa wanashule za msingi ambazo ni mpya hivyo zinauhitaji mkubwa.




0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa