Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza na wananfunzi wa Shule ya Msingi Shinamwendwa (Halmashauri ya Mji Geita) alipokwenda kushiriki kuchmba msingi wa ujenzi wa nyumba pacha ya Walimu shuleni hapo.
Akina mama wa mtaa wa Machinjioni Kata ya Mgusu Halmashauri ya Mji Geita wakishiriki katika ujenzi wa jengo la utawala kwa kubeba maji kupeleka eneo la mradi.Wananchi wwameamua kujenga Shule ya Sekondari kwa kuwa Kata hiyo haina hata shule moja hivyo watoto wanaofaulu ulazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu ya Sekondari katika Kata za jirani.
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kujenga msingi wa vyumba vya madarasa shule ya Sekondari Mgusu baada ya kuzindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na Zahanati Halmashauri ya Mji Geita.Kata ya Mgusu inakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na Shule ya Sekondari.
Mhandisi Modest Apolinary Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita kitoa ufafanuzi kuhusu ramani ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mgusu kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Gabriel kulia ni Herman Kapufi Mkuu wa Wilaya ya Geita.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi amemuagiza Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mji Geita Modest Apolinary kupeleka Wakaguzi wa ndani
wa Hesabu za Serikali Kata ya Mgusu ili wakakague na kujiridhisha na
mapato na matumizi ya fedha mbalimbali katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata
ya Mgusu na Mtaa wa Machinjioni Wilayani Geita.
Mheshimiwa
Robert amesema hayo wakati wa ziara yake Halmashauri ya Mji Geita yenye
lengo la kuzindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na Zahanati
ambapo baada ya uzinduzi kufanyika wananchi wa mtaa wa machinjioni
walimueleza kero ya kutopata taarifa ya mapato na matumizi ya michango
wanayochangia kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa muda mrefu katika
mtaa na kata ya Mgusu.
Akijibu
kero hiyo Mkuu wa Mkoa amesema "Kama kuna kiongozi wa mtaa au Kata
amekula fedha za wananchi hafai kuwa kiongozi serikali itamchukulia
hatua kali za kisheria na atarejesha fedha hizo!, Mkurugenzi leta timu
ya ukaguzi wa hesabu za Serikali ili ikague na kujiridhisha kama kuna
fedha yoyote iliyochukuliwa pasipo maelezo yanayojitosheleza hatua
zichukuliwe haraka kwa wote watakaobainika kuhusika".
Mheshimiwa
Robert ameongeza kuwa ukaguzi huo ufanyike kuanzia mwaka 2014 hadi 2017
kisha apate taarifa hiyo ofisini. Akiwa katika Halmashauri hiyo Mkuu
wa Mkoa amepongeza jitihada zinazofanywa na wananchi za kushiriki katika
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo licha ya kuwepo
changamoto nyingi katika maeneo yao.
0 comments:
Post a Comment