Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kuchanganya mchanga kwenye shughuli ya ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Kazibizyo wakati wa zoezi la uhamasishaji wananchi kujitolea katika uchangiaji wa maendeleo ya ujenzi wa zahanati,vituo vya afya na shule Wilayani Bukombe.
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe ambaye yupo (Katikakati)Josephat Maganga akishirikiana na wananchi pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kufanya shughuli ya kuchanganya mchanga.
Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kujenga msingi wa kujenga zahanati ya kijiji cha Kazibizyo Wilayani Bukombe pamoja na wananchi ambao wamejitokeza kuunga jitihada za serikali za kuleta maendeleo ya huduma za afya maeneo ambayo yanauwitaji .
Katibu tawala wa wilaya ya Bukombe akishiriki zoezi la ujenzi.
NA JOEL MADUKA, GEITA
Mkuu
wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi amewataka wakazi wa kijiji cha
Kazibizyo na Bulama kutumia rasilimali walizonazo ili kuchochea
maendeleo ya vijiji vyao.
Mhandisi
Luhumbi aliyasema hayo katika uzinduzi wa ujenzi wa zahanati kwenye
Kata ya Nga’nzo na Shule kwenye kijiji cha Bulama ili kuwaondolea
wananchi tatizo la kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo.Alisema
matatizo mengi yanasababishwa na baadhi ya viongozi kutowajibika badala
yake kuweka mbele maslahi binafsi.
“Shida
kubwa wananchi tumefanya makosa mengi mno tumekuwa na viongozi bora
viongozi sio viongozi bora viongozi ambao awawezi kuamasisha viongozi
ambao kazi yao ni kula michango ya wananchi viongozi ambao fedha zikija
wanaangalia kupiga kwanza hela ndio wanaleta yale makombo ambayo
yanajenga vitu vibovu vibovu,Sasa viongozi wa namna hiyo hatuwezi
kuwavumilia Geita,ni bora wafungashe virago watafute Mikoa
mingine,kipindi hiki ni kipindi cha kazi kama unaona kazi ni ngumu achia
bodi”Alisisitiza Luhumbi.
0 comments:
Post a Comment