NA JOEL MADUKA
Mkuu
wa Mkoa wa Geita amezindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na
ujenzi wa Zahanati Wilayani Chato ili kupunguza uhaba wa vyumba vya
madarasa na Zahanati Wilayani humo.
Mhandisi
Robert Gabriel amezidua kampeni hiyo kwa kushirikiana na wananchi
kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vymba vya madarasa viwili pamoja
na Ofisi katika shule ya msingi Ilyamchele ambayo inaongezeko la
wanafunzi 2,212 kutoka 1,700. Darasa la pili linawanafunzi 407 ambao
wanasoma kwa awamu mbili hivyo, kufanya shule hiyo kuwa na mahitaji ya
vyumba vya madarasa 28.
Akizungumza
na wananchi baada ya kuchimba msingi Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Serikali
inataka watoto wa Ilyamchele wafanane na watoto wa maeneo mengine kwa
kukaa katika vyumba vizuri vya kisasa vyenye miundombinu ya kutosha na
walimu wa kutosha. Hivyo, ametoa wito kwa wananchi wote kushirikiana na
viongozi wote katika utekelezaji wa miradi hii ili kumaliza uhaba wa
vyumba vya madarasa na Zahanati.
Aidha,
Mkuu wa Mkoa amendelea na ziara hadi kijiji cha Mganza ambapo
ameshiriki katika ujenzi wa kituo cha afya Mganza ili kuona hali ya
wananchi kupata huduma katika vijiji inaimalika kwa kujenga Zahanati na
vituo vipya vya afya.
Miradi
hii inatekelezwa na vikundi vya mafundi walioungana kwa kujitolea
kufanya kazi hiyo pasipo kuwa na malipo isipokuwa kupatiwa chakula
wanapokuwa katika eneo la kazi. Wananchi na wadau wanashiriki kwa kuleta
maji, mchanga, sementi, kokoto na kushiriki katika ujenzi.
Mafanikio
haya yanatokana na juhudi za Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa baada
ya kuwasili mkoani Geita baada ya uteuzi wake aliamua kutoa semina
kuhusu mikakati na njia za kumaliza tatizo la uhaba wa vyumba vya
madarasa na Zahanati kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya,
Wakurugenzi, Maafisa Tarafa, Maafisa elimu wa Wilaya na Makatibu wa
Chama Cha Mapinduzi Wilaya zote.
0 comments:
Post a Comment