Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKUU wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga, ameagiza kukamatwa kwa maofisa ushirika na viongozi wa vyama vya ushirika walioisababishia hasara serikali zaidi ya Sh. milioni 100.
Aidha, amewataka watumishi ambao hawawezi kufuata sheria, taratibu na kanuni za nchi wakabidhi ofisi kwa kuwa serikali haitawavumilia watumishi wanayefanya kazi kwa mazoea na wabadhirifu wa mali za umma.
Alitoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika lililohusisha halmashauri sita za Mkoa wa Geita kwa lengo la kuimarisha vyama vya ushirika kuwa na nguvu ya kukuza uchumi kwa vijana, wanawake na wazee ambao wamekata tamaa baada ya vyama vyao kuteteleka kutokana na utendaji kazi mbovu wa watendaji.
Alisema taarifa za ukaguzi wa vyama vya ushirika 139 kati ya vyama 731 vya mkoa wa Geita vimeshindwa kujiendesha kutokana na utendaji kazi mbovu wa viongozi, usimamizi mbovu wa maofisa ushirika na wanachama kushindwa kurejesha mikopo kwa wakati, hali iliyosababisha serikali kupata hasara ya zaidi ya Sh. milioni 100.
“Yule ambaye hawezi kuwatumikia wananchi kwa tija akae pembeni, serikali ya awamu ya tano haimuonei aibu wala kumlinda mtumishi yeyote anayeshindwa kutekeleza wajibu wake,” alisema Kyunga.
Kaimu Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Charles Malunde, alisema kuporomoka kwa vyama vya ushirika vinavyojihusisha na ukulima, ufugaji, uvuvi, uchimbaji madini, akiba na mikopo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa Victoria kumesababishwa na utendaji kazi mbovu wa viongozi waliochaguliwa.
Aidha, alivitaka vyama vya ushirika kuhakikisha vinawachagua viongozi waadilifu watakaosimamia miradi ya maendeleo ya jamii kwa manufaa ya wananchi na kusema, ili kukabiliana na hali hiyo serikali imejipanga kufufua vyama vya ushirika vinavyofanya kazi kwa kusuasua baada ya kufilisika, kwa lengo la kukuza uchumi wa taifa na kupunguza umaskini kwa wananchi mijini na vijijini na utekelezaji wa mpango wa serikali wa kujenga viwanda.
Aliongeza hatua za awali serikali imezungumza na Benki ya Maendelao ya Afrika ambayo imekubali kukopesha Chama cha Ushirika Chato (BCU) zaidi ya Sh. bilioni nne kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa pamba msimu ujao mwaka 2018/2019 na kuahidi kusaidia ruzuku za pembejeo kwa ajili ya kuinua pamba ambayo inategemewa katika viwanda vya nguo nchini na kuuza nyuzi nje katika Soko la Dunia.
Chanzo:Nipashe

0 comments:
Post a Comment