Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kampuni ya Acacia, kwa
ushirikiano na TANESCO, imejenga kituo cha kupozea umeme kilichopo katika mgodi
wake wa dhahabu wa Bulyanhulu ambacho kimeweza kuongeza uhakika wa upatikanaji
wa umeme katika maeneo ya mgodi huo.
Acacia imewekeza shilingi
bilioni 5.5 katika mradi huo ambao utanufaisha maeneo yanayozunguka migodi ya
Buzwagi na Bulyanhulu na maeneo mengine ikiwa ni pamoja na Kahama, Shinyanga,
Msalala, na sehemu nyingine za Geita.
Ujenzi wa Kituo hicho ulianza
Desemba 2016 na unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.
Haya ni maendeleo makubwa kwa
viwanda na biashara zinazozunguka eneo hilo ambazo zitafaidika na uwepo wa
umeme wa uhakika jambo litakalosaidia kuboresha ufanisi na kuongeza uzalishaji.
“Ujenzi wa kituo hiki utasaidia kupunguza athari zinazotokana na kuongezeka au kupungua kwa nguvu ya umeme katika migodi yetu hivyo kuboresha shughuli za uzalishaji. Wakazi na viwanda vinavyotumia umeme katika wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga na wilaya zingine za mkoa wa Geita zitafaidika na uwekezaji huu pia,” alisema Jiten.
Aliongeza: "Acacia
inajitahidi kuleta manufaa ya kiuchumi ya pamoja kwa jamii zinazotuzunguka na
wadau wake kupitia miradi endelevu."
Wakati wa ujenzi wa kituo
hicho, ajira mbalimbali zilitolewa kwa jamii zinazozunguka mgodi wa dhahabu wa
Bulyanhulu.
Akizungumzia fursa hiyo, David
Nyanda alisema: “tunathamini sana ujenzi wa mradi huu kwa sababu tumepata fursa
za ajira. Japokuwa fursa hizi ni za muda, tunaweza kupata mapato ili kuendesha familia
zetu hasa katika kipindi hiki cha ukame.”
0 comments:
Post a Comment