Home » » MSUKUMA KUWANIA UENYEKITI

MSUKUMA KUWANIA UENYEKITI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  

Ndoto za mbunge wa jimbo la Geita Joseph Kasheku (msukuma) za kuendelea kuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita zipo mikononi mwa kamati kuu ya Taifa ya chama kutokana na kanuni mpya za chama hicho kutoruhusu kiongozi kuwa na kofia mbili za uongozi.
Msukuma ni miongoni mwa wanachama 13 wa CCM ambao wamejitokeza leo kuchukua fomu za kugombea nafasi za uenyekiti ngazi ya mkoa.
Katibu wa CCM mkoani hapa Adam Ngallawa amesema kwa mujibu wa kanuni mpya ya uchaguzi ndani ya chama ya mwaka 2017 mbunge au diwani hapaswi kuomba nafasi yoyote lakini katika mkoa huo wapo waliojitokeza na hatma yao itatolewa na kamati kuu ya Taifa chini ya mwenyekiti wake Rais John Magufuli.
Amesema mbali na Msukuma pia yupo mwenyekiti wa baraza la madiwani wa halmashauri ya mji wa Geita Leornad Bugomola ambae ni diwani wa kata ya Bombambili ambaye ameomba nafasi ya ujumbe wa halmashauri kuu ya taifa .
Ngallawa amewataja wengine ambao wamechukua a fomu ya kugombea nafasi ya uenyekiti kuwa ni Bujukano John ,Paul Luhangija ,John Luhemeja, Deus Lynkando, Ernest Nyororo na Alhaji Kalidushi ambae kwa sasa ni katibu mwenyezi wa chama hicho.
Wengine ni James Msarika,William Misalaba ,Elias Mayila,George Mapalala,Simon Mayengo na Menge Malago.
Amesema katika nafasi ya katibu siasa na uenezi imeombwa na watu saba ambao ni David Azari,Ibrahim Juma ,Agustino Kabelela ,George Mapalala,Lusenga Manjale ,Thobias Meleka na Donald Rubigisa.
Nafasi za ujumbe wa halmashauri kuu ya Taifa imeombwa na wananchama 13 ambao ni Leornad Bugomola ambae ni diwani,Lyidia Bupilipili ambae ni mkuu wa wilaya ya Bunda,Idd Kassim na Musa Derefa.
Wengine ni Mashauri Kaliango Genes Katabalo ,Deusdedut Katwale ,Paul Luhangija, Sashisha Mafue ,Ruvenatus Malecha ,Mapambano Manyungu ,Mary Mazula na Manumba Stephano
“Ni kweli kanuni za uchaguzi haziruhusu mtu mwenye nafasi nyingine ya kisiasa kama mbunge na diwani kugombea nafasi ya uongozi ndani ya chama hawa walichukua fomu na wenye mamlaka ya maamuzi juu yao ni kamatikuu ya Taifa”amesema Ngallawa
Ngallawa aliwataka wagombea hao kuepuka kutoa takrima yoyote kwa wanachama au kuanza kujieleza kwa wananchi na kwamba wagombea wote watajinadi siku ya uchaguzi ambayo ndio siku ya majina ya walioteuliwa kugombea yatatajwa.

Chanzo Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa