Home » » SH10, 000 YAWAPONZA MUUGUZI, MHUDUMU

SH10, 000 YAWAPONZA MUUGUZI, MHUDUMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Geita imewaburuta mahakamani watumishi wawili wa Hospitali ya Wilaya ya Bukombe wakikabiliwa na mashtaka mawili tofauti likiwemo la kuomba na kupokea rushwa ya Sh10,000.
Walioburuzwa mahakamani ni Elizabeth Emanuel ambaye ni muuguzi na David Zakayo ambaye ni mhudumu wa afya katika hospitali hiyo.
Mwendesha mashtaka wa Takukuru mkoani geita, Kelvin Murusuri ameieleza mahakama kuwa washtakiwa wote kwa pamoja waliomba na kupokea rushwa ya Sh10, 000.
Wakisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Veronica Selemani, washtakiwa hao wamedaiwa kutendo kosa hilo Julai 13, kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Katika maelezo ya makossa hayo ilielezwa kuwa wakiwa eneo lao la kazi, washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuomba kiasi hicho cha fedha kutoka kwa mgonjwa aliyeelezwa kuwa ni mzee mwenye umri wa miaka 72 ambaye hata hivyo hakutajwa jina.
Fedha hizo zilidaiwa kuwa ni gharama za mzee huyo kupatiwa majibu ya vipimo alivyochukuliwa alipofika hospitalini hapo kwa matibabu.
Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Wazee ya Mwaka 2003, mgonjwa huyo hakutakiwa kulipia gharama za matibabu.
Washitakiwa wamekana mashitaka na kuachiwa kwa dhamana ya hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh4 milioni na wadhamini wawili hadi Agosti 16, shauri hilo litakapokuja kwa ajili ya kusomewa maelezo ya mashtaka baada ya upande wa Jamhuri kueleza kuwa upelelezi umekamilika.

Chanzo Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa