Home » » KWA NINI MBWA NI RAFIKI?

KWA NINI MBWA NI RAFIKI?

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Kwa nini mbwa ni rafiki?
KUWA rafiki na mbwa yaweza kuwa ni jambo la ‘asili’ na muhimu kwa jinsi walivyokuja kushirikiana maisha na binadamu, wanasema wanasayansi wa Marekani.
Mbwa walijibadili kutoka mbwa mwitu maelfu ya miaka iliyopita. Wakati huo, jeni fulani za kimaumbile ambazo hufanya mbwa apendwe ziliibuka, kwa mujibu wa utafiti.

Hii inaweza kuwapa mbwa sifa tofauti, ikiwa pamoja na shauku ya kuwa na mahusiano na binadamu.

"Utafiti wetu wa maumbile tofauti kwa mbwa wote na mbwa mwitu umetoa ufahamu wa uwezekano kuhusu utu wa wanyama na inaweza hata kupendekeza jeni kama hizo ziweze kuwa na majukumu katika aina nyingine za ndani (labda hata mnyama paka )," alisema Dk. Bridgett vonHoldt wa Chuo Kikuu cha Princeton.

Watafiti walisoma tabia ya mbwa wa nyumbani, na mbwa mwitu wa kijivu wanaofugwa. Walifanya vipimo kadhaa kwa ajili ya kupima ujuzi wa wanyama katika kujaribu kutatua matatizo na utulivu.

Ilionyesha kwamba mbwa mwitu walikuwa wazuri kama mbwa kwa kukabiliana na matatizo, kama vile kurejesha vipande vya nyama zilizosagwa (sausage) kutoka kwenye sanduku la plastiki la kubebea chakula.

Mbwa, hata hivyo, walikuwa na hali ya kirafiki zaidi. Walitumia muda zaidi kuwasalimu watu wageni na kuwatazama, wakati mbwa mwitu walikuwa wachache waliofanya hivyo.

Vipimo vya DNA vilibaini kuwa, kiungo kati ya mabadiliko fulani ya maumbile na tabia kama vile usikilizaji kwa wageni au kuchukulia masuala ya kijamii.

Mabadiliko kama hayo kwa binadamu yanahusishwa na ugonjwa wa kawaida wa maumbile, ambao watu wanapendeza sana.

Dk. Elaine Ostrander wa Taasisi za Afya za Taifa, aliyekuwa mtafiti mshiriki wa utafiti huo, alisema habari hiyo itakuwa muhimu katika kujifunza ugonjwa wa binadamu.

"Uchunguzi huu wa kusisimua unaonyesha matumizi ya mbwa kama mfumo wa maumbile unaojifunza kwa ajili ya tafiti za ugonjwa wa binadamu, inaonyesha jinsi tofauti ndogo ya jeni muhimu katika mbwa husababisha madhara makubwa ya syndromic kwa binadamu," alisema.

Mabadiliko ya mbwa mwitu kuwa mbwa wa kawaida na kumfuata binadamu ulifanywa yapata miaka 20,000 na 40,000 iliyopita.

Hadithi mpya ya ufugaji wa mbwa

Utaratibu huu ulianza wakati mbwa mwitu waliokuwa na uvumilivu kwa wanadamu waliingia katika makambi ya wawindaji ili kula chakula.

Zaidi ya historia, mbwa mwitu hatimaye walikamatwa na kufugwa kisha wakawa mbwa tunaowajua leo, ambayo huja katika maumbo na ukubwa wote, alisema Dr von Holdt.

Utafiti huo umechapishwa katika gazeti la Maendeleo ya Sayansi (the journal, Science Advances).

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa