Frank Mvungi
Mahakama
ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita imemtia hatiani Mgambo wa Mahakama ya
mwanzo Buseresere Bw. Majaliwa Revelian Gwakilala kwa makosa ya kuomba
na kupokea Rushwa kinyume na kifungu cha 15 (1 na 2) cha Sheria ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa.
Kwa
Mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kesi dhidi ya Mtuhumiwa huyo
ilifunguliwa mnamo tarehe 14/1/2016.
Akisoma
hukumu mbele ya mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Augustino Mtaki,
Hakimu Hakimu Mfawidhi wa Wilaya hiyo Mh. Mh. Jovith Kato alisema kuwa
ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na upande wa mwendesha Mashitaka
umethibitisha pasipo shaka yoyote kuwa Mtuhumiwa alitenda kosa hilo.
Ilisisitiza
Sehemu ya Taarifa hiyo kuwa kwa mujibu wa ushahidi Mtuhumiwa aliomba
kiasi cha Tshs. 300,000/= na kupokea kiasi cha Tshs. 100,000/- kutoka
kwa Bw. Reuben Francis Ndimila ili asimkamate mtuhumiwa aliyeruka
dhamana. Taarifa hiyo imeongeza kuwa Mahakama ilimtia hatiani Mtuhumiwa
katika makosa hayo mawili ya kuomba na kupokea hongo.
Aidha
Mh. Kato akitoa adhabu kwa Mshitakiwa alisema, Mshitakiwa anatakiwa
kutumikia kifungo cha miaka Mitatu (3) jela au kulipa faini ya Tshs.
600,000/= kwa kila kosa. Mshitakiwa amepelekwa jela kuanza kutumikia
adhabu hizo kama zilivyotolewa. Kesi hiyo ilisajiliwa mahakamani hapo kama kesi ya Jinai Na. 18/2016 na kusikilizwa na Hakimu Mfawidhi wa Wilaya hiyo.
Mkuu
wa TAKUKURU Mkoa wa GEITA Bw. Thobias Ndaro ametoa wito kwa wananchi wa
Wilaya ya Chato kutoa taarifa mbalimbali za vitendo vya Rushwa na
ubadhilifu katika miradi mbalimbali ya maendeleo na maeneo mengineyo ili
watuhumiwa waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
0 comments:
Post a Comment