Mkuu
wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Amani K. Mwenegoha amewataka waandishi wa habari
nchini kufanya kazi zao kwa ueledi na kwa kuzingatia misingi na maadili ya
taaluma za uandishi wa habari wakati wakifanya kazi za uandishi.
Mhe.
Amani K. Mwenegoha ameyasema hayo jana akitolea ufafanuzi taarifa zilizoandikwa
za upotoshaji zilizotolewa na gazeti la Mwanahalisi iliyoandikwa na
mwandishi Ansbert Ngurumo toleo na: 341 la Mei 30 mwaka 2016 siku ya Jumatatu
ukurasa wa 10 na 11. yenye kichwa cha habari “Ngono na Mwanafunzi yaleta
msukosuko Ushirombo” mimi kama Mkuu wa Wilaya ya Bukombe nimetuhumiwa
kutumia madaraka yangu vibaya kwa kumlinda na kumkingia kifua Afisa Tarafa wa Siloka
Bw. Tumbo John Madaraka.
“Sikuwahi Kupokea barua yeyote kutoka kwa Matayo Paschal wala
kuamrisha akamatwe ,pia sikuwahi kuzungumza na mwandishi
yeyote kuhusu mtoto huyo,wala sijapokea
taarifa kutoka kwa Mkuu wa Polisi Bukombe kuhusu mtoto huyo wala malalamiko
yoyote kutoka kwa wazazi,mlezi au Mwalimu Mkuu wa Shule aliyosoma mwanafunzi huyo” alisema Mhe.
Mwenegoha
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya
Bukombe “amekemea na kulaani kitendo cha mwandishi wa gazeti la Mwanahalisi
kuandika habari bila kuzingatia maadili
ya kiuandishi kwa kufika eneo la tukio na kuonana na walengwa sio kuandika
habari za kupelekewa au kusikia mtaani, angezingatia kupata taarifa kwa pande zote mbili ili kupata
taarifa zenye ukweli,uwazi na uhakika”.
Pia
ametoa wito kwa waandishi wa habari nchini kuwa wazalendo na kumuunga mkono
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika ujenzi wa nchi yetu kwa kufichua uovu
utakaorudisha nyuma maendeleo ya jamii yetu
badala ya kuweka vibonzo visivyowakilisha maslahi ya nchi yetu na kuvunja
moyo juhudi zinazofanywa na Rais wetu za kuinua Uchumi.
Wakati huo huo,
Mkuu wa wilaya ya Bukombe Mhe. Amani K. Mwenegoha amesisitiza wazazi, walezi na
jamii kwa ujumla kutoa taarifa kwa vyombo vya serikali haraka kadri
inavyowezekana inapotokea wana tatizo linalouhusiana na watoto wao wanapokutana
na changamoto ambazo serikali inaweza kushughulikia na imekua ikifanyika hvyo
pale ambapo mzazi,mlezi au jamii inapotoa malalamiko au taarifa kwa Mkuu wa
Wilaya ambapo yamekua yakishughulikiwa na sheria imekua ikichukua mkondo wake.
Imetolewa
na
Ofisi
ya Mkuu wa Wilaya Bukombe
Geita
03
Juni, 2016
0 comments:
Post a Comment