Na Lydia Churi – Geita.
Jaji
Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman amezitaka
Mahakama za mkoa wa Geita kuhakikisha zinamaliza kesi kwa wakati ili
kutekeleza lengo lililowekwa na Mahakama ya Tanzania.
Akizungumza
na watumishi wa Mahakama jana mkoani Geita, Jaji Mkuu alisema Mahakama
ya Tanzania ilijiwekea malengo ya kumaliza kesi katika mahakama zake kwa
wakati kulingana na aina ya mahakama.
Alisema kwa mahakama za Hakimu Mkazi, mahakama za Wilaya pamoja na Mahakama za Mwanzo
lengo lilikuwa ni kumaliza kesi zote ndani ya mwaka mmoja ili kuwafanya
wananchi kuendelea kuwa na imani na mahakama zao kwa kuwa ni zaidi ya
asilimia 90 ya wananchi wanahudumiwa na mahakama hizo.
Jaji
Mkuu alisema kwa mahakama za Mwanzo ambazo ziko 970 nchini kote lengo
lilikuwa ni kuhakikisha hazikai na kesi kwa zaidi ya miezi sita kwa kuwa
ndizo mahakama zinazohudumia wananchi wengi zaidi.
Alisema
ili kuziwezesha Mahakama kutekeleza lengo walilojiwekea, tayari
Mahakama ya Tanzania imeajiri Mahakimu wapya 107 ambao watasambazwa
kwenye Mahakama zote za Mwanzo nchini kwa ajili yakwendakutoa huduma ya
msingi ya mahakama ya kutenda haki kwa wananchi wa Tanzania.
Akizungumzia
suala la utoaji wa nakala za hukumu, Jaji Mkuu amezitaka Mahakama za
mkoa wa Geita kutoa nakala hizo mapema iwezekanavyo ili kutoa haki ya
kukata rufaa kwa wananchi ambao hawakuridhishwa na hukumu walizopewa
katika kesi zao.
Alisema
Mahakama ya Tanzania itaongeza idadi ya Makatibu Mahususi na kuongeza
vifaa katika Mahakama zake ili kuongeza kasi ya uchapaji wa nakala za
hukumu. Alisema asilimia 80 ya bajeti inayotolewa kwa muhimili huo
imetengwa kwa ajili ya kuendesha kesi katika mahakama za Mwanzo, Wilaya
na zile za Hakimu Mkazi.
Jaji
Mkuu anaendelea na zaira yake katika Mahakama Kuu kanda ya Mwanza
ambapo anatembelea mikoa Mwanza, Geita na Mara ili kukagua shughuli za
kimahakama katika kanda hiyo.
0 comments:
Post a Comment