Mmoja wa Mashabiki wa Tamasha la Pasaka pamojana mashabiki wengine waliohudhuria katika Tamasha la Pasaka lililofanyika mjini Geita Mkoani Geita kwenye ukumbi wa Desire wakiimba kwa kuzinguka ukumbi huo wakati mwimbaji Upendo Nkone alipokuwa akifanya vitu vyake jukwaani na kuwafanya wavutiwe na tamasha hilo kiasi cha kushindwa kukaa kwenye viti wakizunguka huku na kule huku baadhi wakiwa wabebeba viti juu juu,
Katika Tamasha hilo mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangachie akizungumza na mashabiki wa muziki wa injili waliohudhuria katika tamasha hilo ameishukuru kampuni ya Msama Promotion na Mkurugenzi wake Bw. Alex Msama kwa kuandaa tamasha hilo kwani hiyo ni fursa pekee ya baadhi ya wananchi wa mkoa wa Geita kumrudia Mungu na kutubu ili kuacha tabia mbaya inayoupaka matope mkoa huo kwa mauaji ya walemavu wa ngozi Albino pamoja na Vikongwe
Waimbaji mbalimbali wameshiriki katika tamasha hilo ambao ni Upendo Nkone, Bonny Mwaiteje, Joshua Mlelwa, Martha Baraka, Jesca BM, Jennifer Mgendi, Mwimbaji kutoka Zambia Ephraim Sekereti, Waimbaji kutoka Nchini Kenya Solomon Mukubwa , na Mtanzania Faustine Munishi pamoja naye Christopher Muhangila.
Matamasha hayo yataendelea kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na keshokutwa litafanyika tamasha lingine kama hilo mjini Kahama mkoani Shinyanga.
Tamasha la Pasaka linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion chini ya mkurugenzi wake Bw. Alex Msama kwa udhamini wa magazeti ya Dira, Dira TV na Dira FM na linafanyika kila mwaka katika kipindi cha sikukuu za Pasaka (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-GEITA)
Mwimbaji Jesca BM akifanya vitu vyake jukwaani.
Mashabiki wake wakiitikia na kuimba kwa hisia wakati mmwibaji huo akiimba jukwaani.
Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama akirekebisha sauti katika mitambo wakati tamasha hilo likiendelea huku DJ akiangalia.
Mama akifurahia uimbaji na uponyaji kutoka kwa waimbaji katika tamasha hilo huku akiwa amemshikilia mtoto wake mchanga.
Maadhi ya mashabiki wa muziki wa injili wakifuatilia waimbaji kwa makini.
Mwimbaji Martha Baraka na kundi lake wakitumbuiza jukwaani huku baadhi yamashabiki wakipata picha kwa simu.
Mwimbaji Jennifer Mgendi naye akafanya mambo makubwa jukwaani kama anavyoonekana.
Mwimbaji Ephraim Sekereti akisalimiana na mdau mkubwa wa Msama Promotion Bw. Silas huku akitaniana na Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangachie wa tatu kutoka kushoto waliosimama mara baada ya kumaliza kuimba.
Mwimbaji Solomon Mukubwa kutoka nchini Kenya akiimba jukwaani huku mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangachie akicheza pamoja na Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama na mashabiki wengine.
Mwimbaji Solomon Mukubwa kutoka nchini Kenya akiimba kwa hisia mbele ya mashabiki wake walioonekana kuhamasika na nyimbo zake.
Mwimbaji Bonny Mwaiteje naye akafanya mambo makubwa jukwaani huku akipewa sapoti na mashabiki wake.
Mwimbaji Bonny Mwaiteje akiwa amewabeba wacheza shoo wake mara baada ya kumaliza kuimba jukwaani hii ilikuwa ni staili ya aina yake.
mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangachie akitoa salamu zake za shukurani kwa kampuni ya Msama Promotion kwa kuandaa tamasha la pasaka katika mkoa wa Geita wilaya ya Geita kwa ni jambo jema kuwahubiria amani wananchi wa Geita ili wamrudie Mungu na kuacha mauaji ya Albino na Vikongwe.
Waimbaji Solomon Mukubwa kulia , Bonny Mwaiteje kushoto wakimpiga tafu Mwimbaji mwenzao Christopher Muhangila katikati wakati alipokuwa akitumbuiza jukwaani.
0 comments:
Post a Comment