Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAZIRI
wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bw. Mwigulu Nchemba amesema hakuna chama
cha siasa ambacho kinaweza kuthaminishwa na maisha ya mwanadamu na
kwamba wananchi hawana sababu ya kupigana na kutoanabugai kwa sababu ya
ushabiki wa vyama.
Ametoa
kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Machi 17, 2016) wakati akizungumza na
mamia ya wakazi wa mji mdogo wa Katoro, wilayani Geita alipopewa nafasi
kuwasalimia wananchi kwenye mkutano wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
"Duniani
kote hakuna chama cha siasa kinaweza kuwa na thamani sawa na maisha ya
mwanadamu au damu ya mwanadamu. Ninazungumza hili nikihusisha na matukio
ya hivi karibuni hapa Geita na kule Tunduma ambako raia wetu walipoteza
maisha kwa sababu ya tofauti za kisiasa, "alisema.
Aliwauliza
wananchi hao ni kwa nini wanapigana hadi kutoana uhai wakati wao
(wananchi) hawaendi bungeni. "Ninyi mnaopigana hakuna hata mmoja wenu
anayeingia bungeni lakini sisi tukikutana kule bungeni tunasalimiana na
kugongeshana glasi.
Akitolea
mfano kauli hiyo, Waziri Mwigulu alisema wakati waneenda kwenye msiba
wa wana CCM waliouawa huku Tunduma, baada ya mazishi yeye na Mwenyekiti
wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe pamoja na wanasiasa wengine walikaa na
kula nyama za kuchoma hadi saa usiku.
"Nini
kinachowafanya muwe maadui wa siasa kiasi hicho?" alihoji na kuongeza:
"Mnasababisha watoto wasio na hatia tena wasiojua siasa wawe yatima.
Duniani siasa hazina tofauti kama zilivyo mechi za mpira. Leo unavaa
jezi hii na kesho jezi ile. Acheni kufanya uadui katika siasa", alionya.
Wakati huohuo,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema atamtuma Waziri wa Nishati na
Madini, Prof. Sospeter Muhongo aende Geita keshokutwa (Jumamosi, Machi
19, 2016) ili akasikilize malalamiko ya wananchi hao juu ya suala la
magwangala.
Magwangala ni mchanga uliochimbwa mgodini na kuchujwa na sasa unatakiwa kuchujwa tena ili utolewe mabaki ya madini na wachimbajiwadogo wadogo.
“Nimemuita
Profesa Muhongo aje na timiu yake ya wakurugenzi pamoja na wataalamu wa
STAMICO ili waje wakamilishe suala hili. Najua lilikwishaanza
kughughulikiwa tangu Makamu wa rais alipopita hapa mwezi uliopita na
sasa nimeambiwa kuwa limefikia asilimia 75 ya utekelezaji,” alisema.
Waziri Mkuu amemaliza ziara ya mkoa huo na anarejea jijini jioni hii.
0 comments:
Post a Comment