Home » » WAZEE GEITA WALIA NA WAJUMBE BUNGE MAALUM

WAZEE GEITA WALIA NA WAJUMBE BUNGE MAALUM

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

BAADHI ya wazee Wilaya ya Geita mkoani hapa wamewalalamikia wajumbe waliopitisha rasimu ya Katiba iliyopitishwa hivi karibuni kwa kutoa mambo muhimu ya wananchi na kuweka yao wenyewe na kwa maslahi yao binafsi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wazee hao walisema kitendo cha wajumbe hao wa Bunge Maalum la Katiba kutoa mambo muhimu kwenye Rasimu ya Jaji Warioba na kuweka yao, si la kiungwana kabisa.
Mmoja wa wazee aliyejitambusha kwa jina la Ramadhani Lucas mkazi wa Geita mjini, alisema wao walitoa maoni yao yanayowahusu na ya kuwasaidia, lakini anashangazwa na kitendo cha lililokuwa Bunge la Maalum kuweka mambo yao kuliko kuweka mambo ya wananchi.
Lucas, aliongeza kuwa maoni aliyoyakusanya Jaji Warioba yalikuwa yanafaa, kwani hayakuwa ya kwake bali ya wananchi, lakini anashangazwa kuona wajumbe wa bunge kuyaacha.
“Jamani sisi Tume iliyoongozwa na Jaji Warioba ilikuja hapa na tukatoa maoni yetu nini tunataka kiwekwe kwenye katiba ijayo, lakini tunashangaa wanaweka ya kwao sijui wana maana gani watu hawa,” alisema Lucas.
Mzee mwingine Juma Shija mkazi wa Katoro, alisema kitendo cha kuwawajibisha viongozi wao wanaposhindwa kufanya kazi zao kilikuwa kizuri, kwani kuna viongozi wa Geita wakichaguliwa wanakwenda kuishi Dar es Salam na kuwasahau wananchi waliowachagua.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa