Home » » BODABODA GEITA WATAKIWA KUFUATA SHERIA

BODABODA GEITA WATAKIWA KUFUATA SHERIA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Bodaboda Geita watakiwa kufuata sheria
JESHI la Polisi kitengo cha usalama barabarani mkoani Geita, limewataka waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda na baiskeli kuacha tabia ya kuingia kwenye barabara kubwa bila kufuata sheria za barabarani.
Akizungumza na Tanzania Daima mjini hapa jana, Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Geita, John Mfinanga, alisema kuwa waendesha pikipiki wanatakiwa kuwa na leseni na kufuata sheria zote za barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.
Mfinanga, alisema kwa kushirikiana na askari wake, wataendelea kuwakamata madereva wote wa vyombo hivyo wasiokuwa na leseni na wasiofuata sheria za barabarani na kuwafikisha mahakamani.
Aliongeza kuwa, wamekuwa wakitoa mafunzo kwa waendesha bodaboda wote mkoani hapa, ili kuwapa uelewa juu ya matumizi sahihi ya barabara na kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika.
“Nawaomba waendesha bodaboda wajitahidi kuwa na leseni na wafuate sheria za barabarani, msako mkubwa wa kuwakamata bodaboda wasiokuwa na leseni na wasiofuata sheria utafanyika, lengo ni kuhakikisha ajali zisizokuwa za lazima zinakwisha katika mkoa huu,” alisema Mfinanga.
Abiria wanaotumia stendi ya Mkoa wa Geita kwa ajili ya kwenda mikoa mbalimbali, wamelishukuru jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kuwondoa wapiga debe, kwani kwa sasa abiria hasumbuliwi kama zamani kwani wanakata tiketi ya gari unalolipenda.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa