Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WANANCHI waliovamia eneo la Nyantorotoro Kata ya Kalangalala Wilaya ya Geita mkoani hapa wametakiwa kuondoka mara moja ili kumpisha mwekezaji mwenye leseni kuendeleza shughuli zake za kuponda kokoto.
Agizo hilo limetolewa jana na Ofisa Madini Mkoa wa Geita, Mhandisi Pius Lobe, wakati akizungumza na wananchi hao mara baada ya mwekezaji huyo Majaliwa Maziku, kulalamika kusimama kwa shuguli zake baada ya wananchi kuvamia na kuanza kuponda kokoto katika eneo lake.
Pius, alisema kuwa mwekezaji huyo ana leseni kumi ambazo zimesajiliwa kisheria na analipia mapato makubwa serikalini, hivyo wananchi hao wanaoponda kokoto ni wavamizi wanaotakiwa kuondoka mara moja, kwani walishalipwa muda mrefu lakini waligoma kuondoka kutokana na maneno ya baadhi ya wanasiasa.
“Jamani mnatakiwa kuondoka mara moja, kwani mwekezaji huyo ana leseni kisheria na mkiendelea kukaa hapa mtakamatwa na mtafikishwa mahakamani hatutaki kutumia nguvu,” alisema Pius.
Naye mwekezaji huyo, Majali Maziku, aliwatafutia eneo lingine wananchi hao ili wasiendelee kuhangaika, ila wengine walikwenda na baadhi kugoma jambo limemsababishia hasara kubwa ikiwamo kuibwa vifaa na mashine zake.
0 comments:
Post a Comment