Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Akizungumza na Waandishi wa Habari waliofika katika eneo hilo, Mwenyekiti wa wachimbaji hao, Elikadi Joshua, alisema tangu wapewe eneo hilo na Ofisi ya madini Mkoa wa Geita mwaka jana, lakini wanachimba kila siku na hawaoni dalili ya kupata dhahabu huku wakitumia gharama zikizidi kuwa kubwa.
Joshua, alisema japo walihakikishiwa na Ofisi hiyo kuwa kuna dhahabu nyingi, wanaona wamedanganywa kwani tangu waanze kuchimba hakuna kitu chochote zaidi ya hasara.
Ofisa Madini Mkoa wa Geita, Injinia Pius Lobe, alipoulizwa kuhusu malalamiko hayo, alibainisha kuwa dhahabu zipo, lakini ni mbali hivyo wanatakiwa kuwa na vifaa vya kisasa.
0 comments:
Post a Comment