Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wakizunguza katika mkutano wa pamoja juzi, ambao ulijadilia
mstakabali wa maisha yao tangu serikali kupitia kwa Mkuu wa Wilaya, Omar
Mangochie kuzuia kufanya shughuli zozote katika maeneo yao, wanakijiji
hao walisema kuwa uongozi wa wilaya umekuwa ukiwadhalilisha mbele ya
wawekezi wa mgodi wa GGM.
Walidai kuwa wamefanya kila jitihada za kuweka mahusiano mazuri dhidi
ya mwekezaji kuhusu malalamiko yao ya kutofanyiwa tathimini na kulipwa
ili waweze kuondoka eneo hilo, lakini uongozi wa serikali hususan mkuu
wa wilaya, umewapuuza.
Wameeleza kuwa wamefikiwa uamuzi wa kupeleka malalamiko yao kwa
Waziri Mkuu kwa vile wanaimani kuwa atawatatulia matatizo yao ili waweze
kurejea katika gurudumu la kuendeleza maisha yao na taifa kwa ujumla.
“Tulimwandikia barua mkuu wa wilaya, kumwomba aje katika mkutano wetu
ili atusikilize matatizo yetu, lakini cha kushangaza aliita viongozi wa
kata na viongozi wa mgodi wa Geita Gold Mine (GGM) na alichokifanya
alitufokea na kutoa vitisho mbele ya wawekezaji hao, hivyo tumeona sasa
tusonge mbele,” walidai.
Wakifafanua zaidi kuhusu sakati hilo, walisema kuwa awali walipewa
amri ya kutofanya shughuli zozote za maendeleo katika maeneo hayo
ikiwemo kulima na uchimbaji madini kama ilivyokuwa zamani, jambo ambalo
limewasabishia umasikini na kushindwa kupata chakula, kusomesha watoto
wao na mahitaji mengine.
“Sasa hivi tunalazimika kuchimba kwa kujifuchaficha ili tuwezo
kuendesha maisha yetu, maana serikali imeshindwa kabisa kutujali sisi
wananchi wake hata kututafutia maeneo mengine ya kuishi,” waliongeza.
Alipotakiwa na gazeti hili kutoa ufafanuzi kuhusu sakata hilo, mkuu
wa wilaya, Omar Mangochie kwa njia ya simu, alikanusha vikali wananchi
hao kutakiwa kuondolewa katika maeneo hayo na kwamba wamezuiwa kufanya
uchimbaji wa madini kwa kuwa ni eneo la mgodi.
“Hawajaambiwa kuondoka, tulichowaambia ni kuacha shughuli za
uchimbaji madini kwa kuwa ni kinyume cha sheria ya madini namba 14 ya
mwaka 2010, kwa sababu kuchimba madini ni lazima uwe na leseni, lakini
pia wanaharibu mazingira,” alieleza.
Hata hivyo, alisema hakumbuki kama aliandikiwa barua ya kualikwa
kwenda katika mkutano huo wa wanachi uliokuwa na lengo la kujadili na
kutatua matatizo yanayowakabili.
Gazeti hili linayo nakala ya barua hiyo ya Julai 5 mwaka huu,
iliyoandikwa na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Magema, Leonard Kalumwa,
ikimwomba mku wa wilaya ahudhirie mkutano wa wanakijiji hicho na
nakala kwenda kwa Ofisa Uslama wa wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya
wilaya, Mkuu wa Polisi wilaya, Ofisa Tarafa ya Geita na Diwabni wa Kata
ya Mtakuja.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment