Home » » VILIO VYATAWALA MAZISHI YA MAMA MKWE,MKWEWE

VILIO VYATAWALA MAZISHI YA MAMA MKWE,MKWEWE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Peter Kakamba
 
Vilio na simanzi viligubikwa katika vijiji vya Ililika na Nyashihima wilayani Geita wakati wa mazishi ya wanawake wawili mama na mkwewe mjamzito waliouawa kwa kukatwa mapanga usiku wa Jumanne katika kijiji cha Ililika.
Miili hiyo ya Nyanjige Mutula (70) na Grace Hayo (18) aliyekuwa mjamzito, ilizikwa katika vijiji tofauti juzi saa 12 jioni kwa hofu ya mwili wa Grace kuharibika baada ya kufanyiwa upasuaji wa kutoa kichanga cha miezi mitano kwenye Kituo cha Afya Kashishi.

Tukio hilo lililoibua hofu kwa  wananchi wa vijiji na kata za Kamena, Nyakamwaga, Lwamgasa na Nyarugusu, walisema mauaji hayo yanahusiana na imani za kishirikina.

Akizungumzia mauaji hayo baada ya maziko, Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ililika, Fabian Mugeta, alisema mikakati ya kuwapigia kura za siri watuhumiwa wa tukio hilo, ilikuwa ikiendelea.

Mugeta alisema ililazimika mwili wa Grace kufanyiwa upasuaji kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini kwao katika kijiji cha Nyashihima na mwili wa binti huyo kuzikwa tofauti na kichanga chake.

Marehemu Mulita alizikwa katika kijiji cha Ililika kitongoji cha Mwabasabi kulikotokea mauaji hayo, na kuhudhuriwa na baadhi ya wananchi, ndugu na viongozi wa kijiji.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Peter Kakamba, alisema mpaka sasa hakuna mtuhumiwa yeyote aliyekamatwa kufuatia tukio hilo la kinyama lililotokea hivi karibuni.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa