Home » » HATARI: BALOZI WA NYUMBA KUMI ADAIWA KUONGOZA KUNDI LA WANANCHI KUTEKETEZA NYUMBA ZA MGANGA

HATARI: BALOZI WA NYUMBA KUMI ADAIWA KUONGOZA KUNDI LA WANANCHI KUTEKETEZA NYUMBA ZA MGANGA




 Hivi ndivyo nyumba zilivyo ungua
 
Na mwandishi wetu Geita 
FAMILIA   ya  Mganga   wa  tiba asilia  Maria  Irigo  (45)  mkazi  wa  mtaa wa  Majengo  kitongoji  cha  CCM  kijiji  na   Kata  ya  Lwamgasa  wilayani  Geita  mkoani  hapa  haina   mahali pakuishi   baada  ya  nyumba  kumi na  moja  za   familia  hiyo  kuteketezwa  kwa   moto  na kundi la    watu (20) wakiongozwa   Burabo  Mapalala  balozi  wa nyumba  kumi  mtaa wa majengo   kitongoji   cha  ccm  kijiji na   Kata  ya   Lwamgasa    kumi na  moja  (11) za  mganga  huyo   wakimtuhumu  kuwa  ni  mchawi  .

Mwenyekiti   wa  serikali  ya  kijiji  hicho   Adam   Mpipi  amesema  kuwa  tukio  hilo  lilitokea  majira ya  saa   4.00 usiku  wa   kuamkia  Agosti  01  mwaka  huu  baada ya  kundi   la  watu  hao  kufika  nyumbani  kwa   mganga  huyo  wakimtuhumu   kuwa ni  mchawi   na  kuteketeza  nyumba   hizo  bila  huruma.

Alisema   kuwa  baada  ya  kupata  taarifa   za  kuwepo  kundi  hilo  ambalo liliandaliwa  kwenda  kwa   mganga  huyo  niliamuwa  kuwa siliana   na mkuu  wa  kituo   cha  polisi   Lwamgasa  ambapo  askari  waliwa hi  kufika  eneo  la  na kufanikiwa  kumuokoa    mganga huyo    lakini kutokana  na  uchache   wao   walishindwa   kuwa dhibiti  watu  ambao  walikuwa   wamejipanga   kumdhuru   mganga  huyo .

Akisimulia  tukio  hilo   Mshindika  Bujilima (17)  ambaye  ni   mmoja  wa watoto  wa  Mganga  huyo  alisema   kuwa  wakati    kundi  la  watu  hao   walipofika  nyumbani  hapo wakiongozwa na balozi    Burabo  pamoja   na   kijana  mmoja  ambaye  anatambulika  kwa  jina  la   Mashaka  na waliaanza  kupekuwa  kila  nyumba   wakimsaka  mganga huyo  huku  wengine  wa kiwa  wamezingira   nyumba  mara  baada  ya  kumkosa  Mganga   huyo  waliamuwa   kuwa  weka  chini  ya  Mshindika   pamoja  na   Dada  yake   Halima   Bujilima  wakiwataka  wawaeleze   mama  yao alipo .

Aidha   alisema  kuwa  baada  ya  kukaidi   kuwaeleza   Mama  yao  alipo  watu   hao  walianza  kuchoma  moto nyumba    wakizidi  kuongezeka  na   kwamba  siku  hiyo  Mama   yao  alikuwa  amepandwa  na  majini  na  alikuwa  hajitambui   la  kini  kutokana   na  uwezo  wa   Mungu  ghafla   alijitambuwa   na  kunakufanikiwa  kutoroka   na  kisha  kuokolewa  na  polisi .

Aliongeza   kuwa  mtu  wa  kwanza   kufika  nyumbani   kwao  siku  hiyo  muda  wa jioni  alikuwa  ni  Mashaka  ambaye  alikaa  hapo   muda  mrefu  kuanzia  saa 12 jioni  wakati  akiwa  bado  Mganga  amepandwa   majini  akataka  kumkamata   Mganga    alipo kaata  kumshika   Masha  alipiga  kelele  na kuondoka  na  kurudi  akiwa  na  kundi  la watu  hao.

,,Kwakweli    watu   hao  walikuwa  wamekusudia   kumua  Mama  kama  wange  mkuta  mimi  wali ni kamata   wakani piga  wakani  weka  chini  ya  ulinzi  ili   ni waambie   mama  alipo   ni kawaambia  sifahamu  alipo  ni  kafanikiwa  kuwatoroka  ni  kamuacha   Dada .

Bi   Maria   amesema  kuwa   siku   hiyo  alikuwa  anaumwa  lakini aliji kuta  amefikishwa  kituo   cha  polisi   Lwamgasa  na  kwamba   kabla  ya  tukio  hilo  walikuwa  na  mgogoro  na   balozi  huyo kwani  siku  zilizopita   ambao  hata  hivyo   walisuruhishwa  lakini  cha kusikitisha  balozi  mwishoni  wa  mwezi  julai   alifanyamkutano  na  kuwa  tangazia  wananchi  kuwa   Mganga  huyo  ni   mchawi  na  kumuambia  matatizo  yatakayo  mpata  serikali  wala  nzengo  haita  husika .

Kufuatia   hali  hiyo  Maria   ameiomba  serikali  kuingilia  kati kumsaidi  pamoja   mashirika   ya  kutetea  haki  za    Binadamu /wanawake  kwakuwa  kitendo  hicho  ni cha  kinyama
Amesema  kuwa   samani  mbalimbali  zimeteketea  ambazo ni  TV , Redio  moja   Baiskel s Akisimulia  tukio  hilo   Mshindika  Bujilima (17)  ambaye  ni   mmoja  wa watoto  wa  Mganga  huyo  aba (7)  Jenereta,  vitanda  Vinne   na   Magodoro,   mabati  tisini (90)   vyote   kwa  pamoja  vikiwa  na  thamani  ya  shilingi milioni  tatu (3).

 Kaimu  ofisa  mtendaji  wa  kata   hiyo  Bw   Erasto    Majura  amethibitisha   kuwepo  kwa  tukio  hilo   na  kuongeza  kuwa   balozi  huyo   katika  tukio  hilo  ana  husika  moja kwa  moja  kutokana  na  kuaanda  kikao  kinyemera  katika  mtaa huo  na  kuhamasisha  wananchi   kinyume  cha sheria   muhtasari  wa kikao tumeukamata  una mhuri  wa  balozi  waeneo  hilo ,Tuna  subiri  jeshi  la polisi lifanye  kazi  yake  balozi   huyo  ni  sawa  na  muuaji  alisema   Kaimu  huyo    Majura.
 
Picha na Habari na Geita yetu Blog

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa