Afisa
Utetezi na Mitandao ya Kijamii toka Shirika la KIVULINI Bi. Khadija
Liganga akifafanua jinsi KIVULINI ilivyoweza kuliinua Shirika la Mtandao
la Watoto la Jijini Mwanza (Mwanza Youth and Chidren Network) na kuweza
kusimamia na kutetea Haki za Watoto katika jiji la Mwanza.
Picha
ya Pamoja ya Maafisa wa Shirika la KIVULINI, Mkurugenzi na Afisa Mradi
wa NELICO, Afisa Maendeleo jamii wa wilaya ya Geita, Muwakilishi wa Plan
International pamoja na Wawakilishi wa Mabaraza ya watoto wilayani
Geita mara baada ya kumaliza ziara ya Kimafunzo katika ofisi za shirika
la KIVULINI.
Shirika
la watoto la New Light Children Center Organization (NELICO) la mkoani
Geita kwa kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya jamii Geita,
limeambatana na wawakilishi 20 toka Mabaraza ya watoto ya kata kumi na
moja (11) za wilaya ya Geita kwa ziara ya kimafunzo katika shirika la
kutetea Haki za Wanawake na wasichana, KIVULINI la mkoani Mwanza.
Ziara
hiyo ya kimafunzo katika shirika la KIVULINI imefanyika hapo jana ikiwa
na lengo la kujifunza namna KIVULINI ilivyosaidia Baraza la watoto
Mwanza kuweza kuratibu na kutekeleza shughuli zake kikamilifu na kuwa
imara zaidi.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo Mkurugenzi wa NELICO Bi. Paulina Alex alisema
kwamba ziara hiyo imelenga kutoa mafunzo kwa mabaraza ya watoto wilayani
Geita juu ya mbinu za kuratibu na kutekeleza miradi mbalimbali lakini
pia kujua mafanikio na changamoto za shirika la KIVULINI katika kupiga
vita ukatili dhidi ya wanawake na wasichana katika mikoa ya kanda ya
ziwa.
“Mabaraza
ya watoto ya Geita bado ni machanga sana na hivyo kufanya safari hii
ya mafunzo kuwa ya muhimu sana. Katika safari hii wawakilishi wa
mabaraza ya watoto wameweza kupata elimu kubwa kutoka KIVULINI na Baraza
la watoto la Mwanza (Mwanza Youth and Children Network) ambalo ni zao
la KIVULINI” alisema Bi. Paulina.
Ziara
hiyo pia ilikuwa na Bw. Maximillian Kitigwa amabe ni mwakilishi toka
shirika la Plan International ambao ni wadau wakubwa wa watoto kwa mkoa
wa Geita pamoja na Afisa Maendeleo ya jamii wa wilaya ya Geita Bi. Emma
Busanji. Watoto hao pia watafanya ziara katika Mkoa wa Arusha kujionea
juhudi za wadau wa maendeleo katika mkoa huo katika kuwaokoa watoto
dhidi ya kufanyishwa kazi hatarishi hasa katika sekta ya madini.
Kivulini
ni shirika lisilo la kiserikali la kutetea na kulinda Haki za Wanawake
na Wasichana. Shirika la Kivulini linahamasisha jamii (Wanawake, Wanaume
na Vijana) kulinda, kutetea Haki za Wanawake na Wasichana kwa kupinga
vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia. Makao makuu ya shirika yapo
jijini Mwanza, Wilaya ya Ilemela, Tanzania.
0 comments:
Post a Comment