TAASISI ya kuzuia na Kupambana na
Rushwa(TAKUKURU) wilaya ya Chato mkoani Geita kwa kushirikiana na wanafunzi wa
vilabu vya wapinga rushwa kwenye shule za sekondari wamelazimika
kujitolea damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaofika katika Hospitali
ya wilaya hiyo.
Hatua hiyo inakuja kufuatia Hosptali hiyo kukabiliwa na uhaba mkubwa wa damu salama hali inayotishia maisha ya wagonjwa wenye mahitaji ya huduma hiyo muhimu.
Hatua hiyo inakuja kufuatia Hosptali hiyo kukabiliwa na uhaba mkubwa wa damu salama hali inayotishia maisha ya wagonjwa wenye mahitaji ya huduma hiyo muhimu.
Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Chato
Dk,Pius Buchukundi, amesema kuwa hali hiyo inekuwa ikisababisha ongezeko la
vifo vya wagonjwa wenye mahitaji ya huduma hiyo kutokana na jamii kushindwa
kuchangia damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya wahitaji.
Aidha Kamanda wa Takukuru wilaya ya
Chato,David Ringia, amesema taasisi yake baada ya kuguswa na tatizo kubwa la
ukosefu wa huduma ya damu salama kwenye hospitali ya wilaya hiyo,na kwa
kutambua kuwa inauwezo wa kutoa elimu kwa jamii mbali na kukamata rushwa,
waliamua kushirikiana na wanafunzi kusaidia kupatikana kwa huduma hiyo muhimu.
Amesema walishirikiana na wanafunzi wapinga
rushwa kutoka shule ya sekondari,Bwina,Wema, Jikomboe na Chato ambapo chupa 17
za damu salama zimepatikana huku akiahidi kuendelea kuielimisha jamii umuhimu
wa kutoa damu kwa ajili ya wengine.
Awali mganga mkuu wa hospitali hiyo,amesema
zaidi ya chupa za damu salama 400 zinahitajika kila mwezi ili kuwahudumia
wagonjwa wanaofika kupata huduma hiyo kila siku badala ya chupa 10 hadi 25
zinazopatikana .
Ametaja baadhi ya magonjwa yanayo changia
uhitaji mkubwa wa damu kuwa ni Malaria,Minyoo,utapia mulo pamoja na baadhi ya
mama wajawazito wanaofika kujifungua na kutokwa na damu nyingi.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment