Uharibifu wa mazingira katika hifadhi mblimbli ikiwemo hifadhi ya mistu wa Rwande katika Halmashauri ya wilaya ya Geita kumesababisha wanyama hatari wakiwemo fisi kutapakaa kwenye makazi ya watu na kusababisha watoto kuuawa kwa kushambuliwa na wanyama hao.
Ofisa wanyamapori wilaya ya Geita, Msese Kabulizina, amekiambia kipindi hiki kuwa uharibifu huo umesababisha wanyama hao kukosa sehemu ya kujihifadhi na kujipatia chakula na hivyo kutakaa kwenye makazi ya watu na kula watoto, mifugo wakiwemo ng’ombe, mbuzi na kondoo.
Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya mtoto,Daniel Dotto(4)mkazi wa Kijiji cha Itale kata ya Katoma wilayani hapa,Februari 10,mwaka huu majira ya saa 1 jioni,kupoteza maisha kwa kuliwa na fisi wakati akitoka kuangalia video na watoto wenzake wane.
Ofisa wanyama pori amesma shughuli za kibinadamu ukiwemo ukataji wa miti ya kuchoma mkaa, mbao na ufugaji umesababisha kutokea kwa matukio ya watoto kuliwa na fisi katika vijiji vinavyopakana na hifadhi ya Msitu wa Ruande.
Katika kipindi cha mwaka jana watoto watano wenye umri kati ya miaka miwili hadi mnne walipoteza maisha kwa kushambuliwa na fisi katika vijiji ya Senga, Katoma, Igate, Lwezera na Nyamboge wilayani Geita vinavyopakana na hifadhi ya Taifa ya Mistu wa Rwande.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment