Home » » RC GEITA! mahakimu tusaidieni kupunguza mlundikano wa mahabusu magerezani‏

RC GEITA! mahakimu tusaidieni kupunguza mlundikano wa mahabusu magerezani‏

Na, Magreth Akinyi Ogolla,Geita yetu blog
           
MKUU wa mkoa wa Geita Magalula Said Magalalula amewataka majaji na mahakimu  wa mikoa ya Mwanza na Geita kuendelea kuhukumu kesi za wananchi wa mikoa hiyo bila kujali masikini au tajiri,na kuacha kurundika mafaili ya kesi kama ilivyosasa.
Bw Magalula aliyasema hayo kwenye mkutano wa chama cha majaji[4]  pamoja na mahakimu zaidi ya sabini kinachojulikana kwa jina la Judges Magistrates Association of Tanzania[JMAT] waliotoka  mikoa ya Mwanza na Geita uliyofanyika  katika ukumbi wa Alifendo Hotel mjini hapa.

Amesema kuwa  mahakimu wengi wamekuwa wakiitendea haki taaluma yao kwa kutoa hukumu za haki ila baadhi yao wamekuwa wakiangalia na kuwapendelea wale watu wenye unafuu wa maisha kwa kutoa hukumu za upendeleo.

"hii ni taaluma yenu ambayo kwa hakika hampaswi kuingiliwa na mtu katika kutoa maamuzi yenu,niseme walio wengi wanafanya haki kwa kutoa maamuzi ambayo hayana upendeleo,lakini wengine wanaangalia huyu masikini ananyimwa haki yake hii hapana" alisema Magalula

Katika kikao hicho aliwataka majaji hao kadhalika na mahakimu  kutumia mkutano huo kujifunza na kurekebisha  mapungufu na changamoto wanazokabiliana nazo ikiwa ni pamoja na kuendelea kuharakisha usikilizwaji na kutoa hukumu  za kesi hizo kwa muda muafaka ili kupunguza mlundikano wa kesi mahakamani na mahabusu huko magerezani.

"tusaidieni kupunguza huu mrundikano wa mahabusu magerezani kwa kusikiliza kesi zao kwa wakati ,zile kesi ambazo ushahidi umekamilika zifanyie kazi tafadhali" aliongeza Mkuu wa mkoa

Mkutano huo uliokuwa na lengo la kutoa elimu jinsi ya  kutatua migogoro ya ndoa pamoja na mirathi.

Naye Aishiel Sumari ambaye ni jaji mfawidhi Mahakama ya kanda ya Mwanza  alimshukuru mkuu wa mkoa wa Geita kwa kukubali kuwa mgeni rasmi na kuahidi kuyafanyia kazi yote yaliyosemwa na mkuu huyo na kuidi kuwachukulia hatua kali  mahakimu watakaobainika wanajihusisha na vitendo vya kuomba na kuchukua  rushwa kwenye mahakama mbalimbali za kanda ya Mwanza.

Aidha Jaji Sumari aliongeza kuwa pamoja na hayo kumekuwa na changamoto mbalimbali zizowakabili ikiwa ni pamoja na kukosa ofisi na vitendea kazi kuwa vichache kwenye mahakama mbalimbali za kanda ya Mwanza na Geita huku akitolea mfano wilaya ya Nyang'wale iliyopo mkoani Geita ambayo haina ofisi hata moja, na kumuomba kusaidiwa pale watakapoomba msaada..

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa