Rodrick Mpogolo
Viongozi hao wa Chadema, UDP, TLP, CUF na NCCR Mageuzi, walisusia kikao hicho mwishoni mwa wiki iliyopita wakidai kudharauliwa na ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo kwa kushindwa kuwalipa posho za vikao hivyo tangu mwaka jana.
Hatua hiyo ilikuja baada ya Kaimu mwenyekiti wa Chama cha UDP wilaya ya Chato, Francis Katambi, kuomba mwongozo juu ya malipo ya kikao hicho kabla ya kufunguliwa.
Baada ya swali hilo, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Clement Belege, alisema malipo ya posho hizo hufanywa na Ofisi ya mkuu wa mkoa na inapotokea mkoa hauna fedha huwasiliana na halmashauri husika ili kusaidia malipo.
Alisema hawezi kuzungumzia posho ya mwaka jana kwa kuwa yeye hakuwa mtumishi wa halmashauri hiyo, licha ya kuthibitisha ofisi ya mkuu wa mkoa imemwandikia barua ili kuwalipa wajumbe katika kikao cha mwaka huu lakini kutokana na halmashauri yake kutokuwa na fedha hapatakuwa na malipo yoyote.
Kauli hiyo ilionekana kuwakera viongozi hao na kulazimika kutoka ukumbini kisha kuondoka hata kabla ya kikao hicho kufunguliwa kwa madai hawawezi kuendela kudharauliwa wakati mchango wao ni mkubwa kujadili na kutoa mapendekezo yao katika bajeti ya halmashauri kabla ya kupelekwa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Wakati viongozi hao wakisusia na kuondoka, mkuu wa wilaya hiyo, Rodrick Mpogolo alikuwa ameketi akisubiri kuruhusiwa kufungua kikao hicho ambacho baadaye kiliendelea kikiwa na wajumbe wachache wakiongozwa na wakuu wa idara za halmashauri hiyo.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment