NA Mwandishi wetu Geita 03.12.2013
MWANDISHI wa
Habari wa Redio Free Afrika,na magazeti ya Mwananchi na Citizen, Mkoa
Geita Bwana Salum Maige amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Geita,
baada ya kuumizwa vibaya kutokana na
kushambuliwa na kundi la askari
Polisi wa Kituo cha Polisi Geita wakati akitoka kutekeleza majukumu yake.
Akizungumza tukio hilo Bwana Maige ambaye amelwazwa
katika chumba namba 4 wodi namda 2
amesema alishambuliwa juzi majira ya saa
moja na dakika 45 usiku, na kundi la
askari polisi zaidi ya wanane karibu na zilipo ofisi za
polisi mkoa pamoja na ofisi ya mkuu wa mkoa.
Amedai siku hiyo
akiwa katika maeneo hayo wakati akielekea nyumbani kwake mtaa wa Bomani, alikutana na kundi hilo la polisi walikuwa na gari lenye namba
za usajili PT 1998 OCD GEITA, ambapo baadhi yao walishuka kutoka kwenye gari
na kumueleza kwamba yuko chini ya
ulinzi anahitajika polisi.
Amesema alilazimika
kuwauliza polisi kosa lililosababisha
ahitajike polisi, lakini badala ya kumjibu walimshika na kumfunga pingu mikononi kisha kumtupia
ndani ya gari na kuanza kumshambulia kwa
vipigo.
Maige amejeruhiwa
vibaya jicho la upande wa kushoto
ambapo kwa mujibu wa Daktari
aliyemfanyia uchunguzi kwenye jicho amesema amepasuka mishipa kwa ndani
kutokana na kipigo hali iliyosababisha damu kuvujia ndani ya jicho.
Akifafanua Maige amesema katika siku za hivi karibuni amekuwa katika
mgogoro wa kifamilia na Mkewe, hali iliyosababisha mkewe kwenda
kumshitaki polisi, ambapo polisi waliamua kwenda kumkamata
kabla hata ya kumfungulia mashitaka, na baada ya kufikishwa polisi ndipo
alipomkuta mkewe na kuanza kumfungulia
mashitaka.
Hata hivyo katika hali
ya kushangaza pamoja na kujeruhiwa polisi walikataa kumpatia fomu
namba tatu (PF3) kwa ajili ya kwenda kupata matibabu hali iliyosababisha
kushindwa kupata matibabu, hadi jana
asubuhi ambapo baadhi ya waandishi walilazimika kwenda naye polisi na kudai
apatiwe fomu hiyo na kwenda kupatiwa matibabu.
Kamanda wa polisi Mkoa
Geita Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Leonard Paulo hakupatikana
jana kuzungumzia tukio hilo la shambulio
dhidi ya Mwanahabari huyo, lakini Kaimu wake ACP Pudensiana Protas
alithibitisha kupewa taarifa juu ya
kukamatwa kwa mwandishi huyo lakini
hakujulishwa juu ya kushambuliwa kwake.
Hata hivyo baada ya
kuoneshwa picha za majeraha ya mwandishi huyo ofisini kwake alionekana
kushituka na kuahidi kwenda hospitalini
kufanya mazungumzo na mwandishi huyo, na kwamba
baada ya hapo atafuatilia suala hilo kabla ya kulitolea maelezo ya kina.
"mfukoni nilikuwa na kamera,voce recoder na hela elfu kumi na sita
na wakati wananibeba vilidondoka nikawaambia jamani nimedondosha vitu vyangu, badala ya kunisikiliza nilinaswa kofi na askari mmoja,sijui kama kuna mtu alivichukua au lahh!" alidai Maige
Imeelezwa kuwa muda mfupi kabla ya tukio la kumshambulia Mwandishi huyo,gari lililotumika alikikuwa nalo Mkuu wa polisi wilaya Mrakibu mwandamizi wa polisi Bwire ambaye alikuwa akiendesha mwenyewe maeneo ya mtaa wa Nyerere karibu na "Classic Pub"
Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia baadhi ya vigogo wakipishana maeneo ya hospitali ya wilaya akiwemo Mkuu wa upelelezi wa jinai mkoa wa Geita Kamishina wa polisi Franco Kibona wakifanya jitihada za kumbembeleza Mwandishi aliyejeruhiwa ili yaishe, huku akikiri kuwa vijana wao walifanya kosa kumpiga
" unasikia Maige hawa vijana wetu wamekosea sana maana wewe hakuna hasiyekufahamu,naomba utusamehe kwa hili wewe ni mtani wangu" alidai Mkuu wa upelelezi mkoa.
Habari na Geita yetu Blog
0 comments:
Post a Comment