zaidi ya wanafunzi 500 wanaosoma shule ya msingi Nyang’homango katika
kata ya Ilemela wilayani Chato mkoani Geita hawana mahala pa kujisaidia
baada ya vyoo walivyokuwa wakitumia kutitia na kubomoka kutokana na
kujengwa chini ya kiwango.
Hali hiyo imeelezwa kwenye mkutano mkuu wa dhalula wa kijiji na mwalimu
mkuu wa shule hiyo Bw. Gilbert Edward ambaye amesema hali hiyo
inahatarisha maisha ya wanafunzi hao.
Amesema vyoo hivyo vilijengwa mwaka 2002 na serikali kupitia mpango wa
HESAWA lakini havikuwa na ubora kutokana na kujengwa bila kuwekewa nondo
hali ambayo imesababisha vititie.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Ilemela wilaya Chato Bw. Ismail Luge
amewataka wananchi hao kuchukua hatua za haraka kujenga vyoo vingine
hali itakayosaidia wanafunzi hao kujisaidia watakapokuwa wamefungua
shule.
Ili kuunga juhudi hizo za ujenzi wa vyoo vipya diwani Luge amechangia
mifuko mitano ya saruji huku wanakijiji wakitakiwa kuchangia shilingi
13,000 kwa kila mwenye uwezo wa kufanyakazi kwa lengo la kukamilisha
shilingi milioni tatu kwa ajili ya ujenzi huo.
Home »
» SHULE YENYE ZAIDI YA WANAFUNZI 500 HAINA VYOO GEITA WANAFUNZI
0 comments:
Post a Comment