Marehemu ni mzaliwa wa Morogoro
Huyu ni mzaliwa wa Geita
Na Denice Stephano,Geita Yetu Blog
WAKATI serikali kupitia wizara ya elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini ikifanya jitihada za kuakikisha inaboresha sekta ya elimu na kuhakikisha Matokeo makubwa sasa yanapatikana (BIG RESULTS NOW) katika sekta hiyo,idara ya elimu wilayani Geita kumedaiwa kuwepo baadhi walimu ambao hawana taaluma hiyo.
Huyu ni mzaliwa wa Geita
Na Denice Stephano,Geita Yetu Blog
WAKATI serikali kupitia wizara ya elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini ikifanya jitihada za kuakikisha inaboresha sekta ya elimu na kuhakikisha Matokeo makubwa sasa yanapatikana (BIG RESULTS NOW) katika sekta hiyo,idara ya elimu wilayani Geita kumedaiwa kuwepo baadhi walimu ambao hawana taaluma hiyo.
Hivi
karibuni kumekuwepo taarifa za kuongezeka kwa wanafunzi wasiojua kusoma
na kuandika mara baada ya kumaliza elimu yao ya msingi huku wakiwa
wameshinda kwenda sekondari,jambo ambalo limekuwa likishangaza jamii.
Chanzo cha kuaminika kiliidokeza Geita yetu Blog kuwa Mwalimu huyo alikuwa akifanya hivyo kutokana na kuwa na mahusianao na kigogo mmoja wa elimu wilayani hapa ambaye pia katika barua ya kumthibitisha kazini na ile ya kumpandisha daraja ndiye aliyesaini jambo ambalo liliwatia hofu Mratibu Elimu kata na Mwalimu mkuu kumfuatilia mwalimu huyo.
" Mwl Revina Ignatus sio jina lake la kwake ni Julieth Ng'omang'o nyumbani kwao wanamwita "Yulita" amezaliwa Kijiji cha Bungw'angoko tarafa ya Kasamwa,amesoma Bungw'angoko shule ya msingi na baada ya kumaliza alienda Bukumbi Sekondari mkoani Mwanza ambapo aliacha shule akiwa kidato cha kwanza kwa kuumwa macho na kurudi kijijini kwao baadaye akapata kazi ya upishi katika mgodi wa dhahabu wa Geita na watu wanamjua wengine wakisikia ni mwalimu watashangaa" kilisimulia chanzo chetu
"amepika pika chakula mgodini hadi 2007 ndio akaajiriwa kiujanjaujanja,alikuwa na dada yake(kwasasa ni marehemu) ambaye yeye kweli alikuwa amesoma ualimu na alikuwa anafundisha Nyanza Shule ya msingi hapa mjini,huyu dada alikuwa anaitwa Mwl Pili Ng'omango,huyu ngugu yake alifariki sasa huyu wakati anafuatilia mirathi ndipo akaanza uhusiano na kigogo hapa wilayani,naona amemfurahisha akaamua ampe jina la mtu ambaye amekwishafariki ambalo ni Revina Ignatus na kupelekwa huko Ludete ambako hajulikani" kiliongeza chanzo hicho
Aidha Geita Yetu ilimtafuta Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu,wilayani Geita Bw.Solla Tandas ambaye katika barua ya kumthibitisha kazini mwalimu huyo na ile ya kumpandisha Daraja ndiye aliye saini barua zote,ili kupata ufafanuzi,hata hivyo baada ya kumdokeza ageuka bubu na kudai yeye sio mwajiri hivyo atafutwe mwajiri ndiye anajua.
"mimi sio mwajiri! mwajiri hapa ni mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya,nenda kwake au umtafute yeye ndiye ana majibu sahihi ila mimi ninachokifahamu mtumishi yeyote anayefariki huwa tunamfuta" alieleza Tandas
Jitihada za kumpata Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Bw.Ally Kidwaka zilifanikiwa na baada ya kuelezwa juu ya utata wa ajira ya mwalimu Revina Ignatus,ambapo alimwita Afisa Elimu Wilaya,Bw.Ishengoma Kyaruzi ili waondoke wote hadi kituo anachofanyia kazi Mwalimu huyo ili wajiridhishe.
Katika safari hiyo waliambatana na Geita yetu na kufanikiwa kufika shuleni hapo majira ya saa 6:15 mchana na kupokelewa na mwalimu mkuu wa shule hiyo Bi.Shida Ndaro, huku mwalimu huyo akiwa hayupo kazini kwa madai alikuwa anaumwa.
Mara baada ya kupokelewa mkurugenzi alieleza sababu za yeye kufika shuleni hapo kuwa alitaka ajue kama kweli kuna mwalimu ambaye anafundisha ila hajasoma ualimu na ameajiriwa" tumekuja hapa ili tujue ukweli kama kuna mwalimu anafundisha na hana taaluma ya kufundisha,hapa kwako? alieleza Kidwaka
Katika kujibu swali la mkurugenzi mwalimu Ndaro,alidai yeye anachojua waliopo pale ni walimu halali maana,maana amewapokea wakiwa na barua toka wilayani "kila mwalimu anayekuja kuripoti hapa hufika na barua toka wilayani kazi yangu hapa nai kuwapokea na kuwapangia kazi hivyo najua ni walimu wamesoma ualimu" alijibu Ndaro
Naye afisa elimu wilaya aliyekuwa ameambatana na Mkurugenzi huyo alitaka kujua kama mwalimu mkuu huwa anamkagua mwalimu wake,hata hivyo Mwalimu Ndaro alijitetea na kudai yeye huwakagua mara kwa mara walimu wake " ila katika kumkagua mwalimu naweza nikakuta ameazimia,ameandaa somo inavyotakiwa lakini mwandiko sio wake" aliongeza Ndaro
Katika mahojiano na mwalimu wa taaluma shuleni hapo,yeye alikiri kuwa mwalimu Revina uwezo wake ni mdogo na baada ya kugundua hivyo alimbadilisha kutoka darasa la tano alikokuwa anafundisha somo la Kiswahili na kumpeleka darasa la kwanza
"sisi wote hapa tupo kazini kila mtu anajua ameingia vipi kazin!i sasa ukimfuatilia sana mtu unaweza ukaonekana mbaya,baada ya wanafunzi wa darasa la tano kumlalamikia tuliamua kumbadilisha na kumpeleka la kwanza,huyu kabisa ile 'knowledge' ya ku-'deriver material' kwa watoto hana kabisa ila tufanyeje? alilalamika mwalimu wa taaluma
Hata hivyo baada ya kumkosa shuleni hapo ,Afisa elimu aliacha ujumbe shuleni hapo kwamba akipona afike ofisini kwake mara moja akiwa na vyeti halisi
Kwasasa ni mwezi mmoja toka afisa elimu na mkurugenzi watoe maelekezo hayo mwalimu huyo akiwa ameshindwa kutekeleza huku kukiwa na taarifa kuwa siku hizi haendi kazini,jambo ambalo Mkurugezi ameamua kusitisha mshahara wa mwalimu huyo na kuanza kufanya uchunguzi juu ya ajira yake na wote waliohusika na kwamba ikithibitika walidanganya,hatawachukulia hatua bila kujali mkubwa wala mdogo.
Ikumbukwe kuwa Mwalimu huyu ameajiriwa toka 2007 na amelipwa mshahara hadi 2010 bila kufanya kazi yoyote akiwa nyumbani,amewalisha watoto sumu ya kutosha toka 2010-2013 maana sio mwalimu,wanaosoma shule hizi ni watoto wa wakulima,ndio madaktari na wataalam wa baadaye,Geita Yetu Blog inampongeza Mkurugenzi Ally Kidwaka kwa hatua alizochukua.
KAMA KUNA GAZETI LINATAKA TUMIA HABARI HII TUWASILIANE KWA NAMBA 0654221465
GEITA YETU BLOG
0 comments:
Post a Comment