Home » » WANANCHI WA BUKOMBE KUNUFAIKA NA UMEME.

WANANCHI WA BUKOMBE KUNUFAIKA NA UMEME.


 
NA MARCO KANANI
BUKOMBE.
WANANCHI wapatao 7,682 wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita,
watanufaika na umeme watakapounganishiwa nishati hiyo, baada ya kukamilika kwa
mradi wa awamu ya kwanza.
 
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, juzi alisema
kuwa wananchi hao waka mkao wa ‘kiumeme’ kwani tathmini ya ya mazingira imeisha
fanyika na kufikia Novemba 25 mwaka huu, nguzo za umeme zitaanza kumwagwa ili
ujenzi uanze mara moja.
 
Masele aliyepewa nafasi na Rais Dkt Jakaya Kikwete kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika mjini hapa ili awalezee wananchi wa Bukombe, lini
umeme utawafikia, alieleza kwamba, serikali ya awamu ya nne inafanya kila
jitihada kubwa kuhakikisha umeme unawafikia wananchi wengi nchini ili wakuze
vipato vyao kwa kutumia nishati hiyo.
 
“Serikali inafanya jitihada kubwa kuwafikishia wananchi wengi
nishati ya umeme ili muweze kukuza vipato vyenu kutojkana na shughuli za
kiuchumi mnazozifanya kwa kutumia umeme sambamba na kuwatafutia wachimbaji
wadogo vifaa vya uchimbaji nao waendeshe uchimbaji wa kisasa.” Alieleza.
 
Alifafanua kwamba, lengo la serikali ya CCM ni kuinua pato
la wachimbaji hao na kudai “Serikali imedhamiria kuona wachimbaji wadogo wa Tanzania
wanachimba kwa tekonolojia ya kisasa.”
 
Geita yetu Blog 

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa