Home » » JK AKERWA NA UPUNGUFU WA DAWA KATIKA HOSPITALI.‏

JK AKERWA NA UPUNGUFU WA DAWA KATIKA HOSPITALI.‏

NA MARCO KANANI
GEITA.
 
RAIS Dkt Jakaya Kikwete amesema atashughulikia tatizo la
upungufu wa dawa katika hospitali za mkoa wa Geita ili zifike kwa wakati,
wananchi wavute subira.
 
Dkt Kikwete alitoa ahadi hiyo juzi mjini Bukombe wakati akihutubia
mkutano wa hadhara kwenye kituo cha mabasi cha wilaya hiyo, ikiwa ni siku ya pili
ya ziara yake mkoani Geita.
 
Rais alisema ili kujua nani anakwamisha dawa kufika mapema. Suala
hilo aachiwe yeye na tayari ameisha muagiza Mtunza Stoo ya madawa Kanda ya
ziwa, akutane naye mjini Geita kupata ufumbuzi.
 
“Suala la upungufu wa dawa niachieni mimi, nimemuagiza
mtunza stoo ya madawa kanda ya ziwa tukutane naye mjini geita wakati wa
majumuisho ili anipe taarifa za kueleweka.”  Alieleza Dk Kikwete huku akionekana kukerwa na
tatizo hilo baada ya Mbunge wa jimbo hilo Kulikoyela Kahigi kudai hospitali ya
wilaya hiyo haina dawa.
 
Akizungumzia tatizo la Ukimwi, Rais alisema ameshtushwa na kiwango
klikubwa cha maambukizi wilayani Bukombe na kuwataka wananchi wachukue hatua
zinazostahili kwani taarifa aliyopokea inaonyesha kiwango hicho kinafikia
asilimia 6.3, kikizidi cha taifa ambacho ni asilimia 5.3.
 
“Maambukizi ya Ukimwi yamenishtua katika wilaya yenu,
chukueni tahadhari, tumieni kinga vinginevyo tutaendelea kupoteza watu wengi,
acheni kufanya mzaha na ukimwi kwa kufanya ngono holela.” Aliasa Rais.
 
Kwa mujibu wa takwimu za mambukizi ya Ukimwi za wilaya hiyo,
watu 8,100 wambainika kuwa na maambukizi hayo ambapo kati yao 5,500 wameanza
kutumia dawa za kurefusha maisha. 
 
Akizungumzia tatizo la maji wilayani humo, Rais alisema anaendelea
kuwasiliana na wafadhili mbalimbali ili wasaidie kuondoa kero hiyo na kwamba
anatarajia kwenda nchini India kufuatilia wafadhili ili kuipatia maji ya
uhakika mikoa ya Geita, Simiyu, Shinyanga na Tabora huku maeneo mengine nchi
nayo yakiendelea kutafutiwa ufumbuzi.
Geita yetu Blog 

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa