Home » » MWANDISHI ANUSURIKA KUPIGWA NA MFANYABIASHARA WA MADINI‏

MWANDISHI ANUSURIKA KUPIGWA NA MFANYABIASHARA WA MADINI‏

Na Mwandishi wetu Geita Yetu.
USALAMA wa waandishi wa habari umezidi kuwa mdogo pindi wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao,hali inayosababisha hofu miongoni mwao.
 
Hatua imekuja baada ya mwandishi wa habari wa gazeti la Mzawa wilayani Geita,Alphonce Kabilondo kunusurika kupigwa na mfanyabiashara wa dhahabu mbele ya kituo cha polisi cha Katoro wilayani hapa wakati akiwa katika majukumu yake ya kazi baada ya kutokea ajali iliyohusisha gari la mfanyabaishara huyo.

Kabilondo alikumbana dhahama hiyo majira ya saa 8 mchana alipokuwa akifuatilia tukio la ajali ya barabarani iliyotokea leo(jana) na kusababisha vifo vya watu wawili akiwemo mwendesha bodaboda.

Mfanyabishara huyo anayefahamika kwa jina moja la Bore mkazi wa Katoro akiwa katika kituo hicho cha polisi baada ya kugundua kuna waandishi wa habari na ndipo alitoka ndani na kumfuata mwandishi huyo kwa lengo la kumpiga lakini alijihami kwa kumkwepa.

Hata hivyo aliwazuia waandishi wa habari kulipiga picha gari lake lenye namba za usajili T 910 BSN lililosababisha ajali hiyo baada ya kugongana na pikipiki namba T 579 BUV iliyokuwa ikiendeshwa na Athuman Mrisho(29) akiwa amembeba abiria Dotto Paulo(30)ambao wote walifariki papo hapo.

Aidha katika hali isiyotarajiwa mfanyabiashara huyo alidai kumshughulikia mwandishi yeyote atayeandika habari kuhusiana na ajali hiyo kwa madai kwamba polisi mkoani hapa akiwemo kamanda wa polisi Leonard Paulo liko mikononi  mwake.

‘’Kaandike utaona,nitakushughulikia vibaya sana.hunifanyi kitu polisi wote hapa hawanifanyi kitu hata kamanda nafahamiana naye,dhubutu uone’’alisikika Mfanyabiashara huyo mbele ya polisi.

Kiburi hicho kinatokana na mfanyabiashara huyo mwaja jana kutoa msaada wa kulikarabari gari la polisi la kituo hicho na kwamba mwandihsi huyo alipokuwa akitishiwa kupigwa hakuna polisi aliyejitokeza kumsaidia.

Akisimulia tukio hilo Kabilondo alisema ameshangazwa na polisi kushindwa kumchukulia hatua kigogo huyo wakati anataka kumpiga

"huwezi amini yaani mtu ananitishia mbele ya kituo cha polisi na askari alafu anaachwa,mambo gani sasa,polisi wanalinda nini! imeniuma sana,mtu kuwa na hela tayari anaweza fanya kitu anachokitaka? alisema Kabilondo

Ajali hiyo imetokea Jana majira ya  saa 6 mchana eneo la Kasesa kata ya Kaseme barabara itokayo Katoro wilayani Geita kwenda Lulembela wilayani  Mbogwe mkoani Geita.

Kamanda wa polisi mkoani Geita Paulo alipotafutwa kwa njia ya simu kuzungumzia madai ya mfanyabaisha huyo kuliweka jeshi la  polisi mikononi mwake,simu yake iliita bila kupokelewa,Ingawa jeshi la polisi wilaya ya Geita limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa