BARAZA
jipya la madiwani katika halimashauri mpya ya wilaya ya Nyang'whale
mkoani Geita wamemtaka mkuu wa polisi mkoa wa Geita kumuamisha askari
mmoja mmoja wa kituo cha polisi Msalala ambaye amekuwa akiwanyanyasa
wananchi na
kubambikiza kesi mara kwa mara na kuomba rushwa kwa baadhi ya
wananchi.
Wito
huo umetolewa hivi karibuni na baadhi ya madiwani kwenye baraza lao la
kwanza lilofanyika katika ukumbi wa halimashauri hiyo, kauli hiyo
imekuja baada ya kuwepo asikari mmoja aliyefamika kwa jina moja la Frank
kuwanyanyasa wananchi na kuwambikiza kesi na kuwaomba rushwa.
Wamedai
kuwa askari huyo amekuwa ni kero kubwa kwa wananchi kwa kubanbikiza
kesi na kuwaonba ruswa wanapokosa kumpa pesa na huwabambikiza kesi za
unyang'anyi wa kutumia silaha ambazo hazina dhamana na huku akifanya
kazi za barabarani kama
Traffic ikiwa ni sehemu moja wapo ya kujipatia kipato.
Imeelezwa
kuwa askari huyo anayedaiwa kuhishi nyumba ya kulala wageni kwa kipindi
cha miezi [8]toka alipohamia wilayani humo akitokea wilayani Chato kwa
tuhuma za rushwa hali iliyosababisha madiwani kuhoji anapata wapi pesa
za kulipia gest shilingi [35ooo]kwa siku.
Mkuu wa polisi wilaya ya Nyangwhale Mrakibu wa polisi Bw, Madalali Msekela
akizungumza kwa njia ya simu kupitia simu yake ya kiganjani alikiri
kupokea malalamiko juu ya askari huyo na kudai tayari amelifikisha kwa
viongozi wake wa mkoa kwa ajili ya maamuzi.
"malalamiko
hayo yapo tayari nimeyapata,ila siwezi kuzungumza lolote maana tayari
nimelifikisha kwa bosi wangu huko mkoani,na linafanyiwa uchunguzi,kama
unaweza wasiliana na kamanda yeye atalitolea ufafanuzi"alisema Madalali.
Hata
hivyo juhudi za kumtafuta kamanda wa mkoa Geita Kamishina msaidizi wa
polisi, Leonard Paul ili kulitolea ufafanuzu suala hilo hazikuzaa
matunda kutokana na simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa na
baadaye kuzimwa na baadaye mwandishi alipata taarifa kuwa kiongozi huyo
alikuwa busy na shughuli za harusi ya mwanaye iliyofanyika
26/10/2013.
0 comments:
Post a Comment