Home » » HOT NUUZ, MAKUBWA MENGINE YAIBUKA GEITA(PICHA):KIJANA ALIYEKUFA KWA KUJINYONGA MWAKA MMOJA ULIOPITA,AONEKANA TENA AKIWA HAI NDUGU WATHIBITISHA KUWA NDIYE YEYE!‏

HOT NUUZ, MAKUBWA MENGINE YAIBUKA GEITA(PICHA):KIJANA ALIYEKUFA KWA KUJINYONGA MWAKA MMOJA ULIOPITA,AONEKANA TENA AKIWA HAI NDUGU WATHIBITISHA KUWA NDIYE YEYE!‏

 Kijana Mgonda Thomasi (22) akiwa katika gari la Polisi Mara baada ya kuonekana akiwa hai  huko Geita.
Mamia ya wanakijiji huko Geita wakimshangaa kijana Mgonda Thomasi (22) aliye Fariki dunia kwa kujinyonga huko Geita na sasa kuonekana akiwa hai kabisa.
 Baadhi ya watu wakiwa wamemshikiria kijana Mgonda Thomasi (22) Baada ya kuonekana akiwa hai
 Huyu Ndiye  kijana Mgonda Thomasi (22) akiwa ameonekana hai huku Mwaka mmoja uliopita alikuwa ni Marehemu
Wanakijiji Mbalimbali wakiwa wamemshuhudia kijana Mgonda Thomasi (22)  akiwa hai baada ya kufufuka  kutoka mwaka jana 2012.

 ******************
 Habari na Denice wa Geita yetu Blog.
KWA kipindi cha mwezi mmoja katika mkoa wa Geita matukio ya kusisimua ya watu wanodaiwa kufa na baadaye kuonekana wakiwa hai yamezidi kupamba moto baada ya kijana  mwingine anayedaiwa kufa kwa kujinyonga mwaka mmoja uliopita  kuonekana akiwa hai kijijini kwao Lumasa wilayani Chato mkoani Geita.

Tukio hili limetokea ikiwa ni siku chache baada ya mtoto Shabani Maulidi (15) kuonekana baada ya kufariki miaka miwili na nusu iliyopita na kuonekana tena akiwa hai mjini Geita.

Aidha kijana Mgonda Thomasi (22) ambaye ameonekana tena anayedaiwa kufariki kwa kujinyonga mwenyewe Mei,25 2012 kwa kutumia kamba za viatu ambapo alikutwa akiwa amening'inia kwenye mti wa mwembe ulipo jirani na nyumba yao wanayoishi.

Oktoba 18 majira ya saa tisa alasiri katika Kijiji cha Lumasa Kata ya Butengo Lumasa Wilayani Chato  kijana huyo kuonekana akiwa hai   jirani na nyumbani kwao na kufanya mamia ya wakazi wa kijiji hicho na jirani kumiminika kushuhudia tukio hilo.

Baba huyo alisema kuwa siku ya tukio hilo walikuwa na sherehe ndogo ya kifamilia ya kushirikishana mambo ya kiukoo ambapo marehemu siku hiyo alikuwa mchangamfu na ndiye alikuwa anaongoza vyombo vya muziki vilivyokuwa vikitoa burudani katika sherehe hiyo.

Akizungumza kwa masikitiko baba mzazi wa kijana huyo Thomsi Msalaba (60) alidai mwanaye alifariki kwa kujinyonga mwenyewe kwa kutumia kamba ya viatu na kujining'iniza kwenye mti wa mwembe uliopo karibu na nyumba yao.
Alisema baadaye walimkosa kwa muda mtoto huyo bila kujua alikoenda ndipo walipoanza kumtafuta kisha kumuona akiwa amejinyonga juu ya mti wa mwembe akitumia kamba ndogo ya viatu akining'nia  huku akiwa amekata roho pasipo kuacha ujumbe wowote.

Alibainisha kuwa ndugu na majirani walishikwa na mshangao mkubwa kisha wao kama familia walivitaarifu vyombo vya dola ambavyo vilifika na kutimiza taratibu za kisheria kisha waliruhusiwa kuuzika mwili wa mtoto wake tarehe 29.05.2012.

Akizungumzia jinsi mtoto huyo alivyoonekana baba huyo alisema juzi tarehe 18.10.2013 saa tisa kamili alasili kijana huyo alionwa na majirani karibu na nyumbani kwao kisha walipiga yowe na watu kukusanyika ambapo wote walimtambua kuwa ndiye Thomas.

Mdogo wa kijana huyo Mussa Thomas ambaye aliwahi kufika eneo la tukio baada ya kusikia kelele alisema alimtambua moja kwa moja kaka yake Thomas kutokana na jinsi anavyofanana na mama yake Martha Kitobelo (51) pia aliliona kovu la kuungua kwa moto alilokuwa nalo katika mkono wake wa kushoto kitu ambacho hata baba yake alikithibitisha .

"Huyu ni kaka yangu kabisa sura yake pamoja na alama ya kovu la kuungua mkono wa kushoto ipo pia anafanana kabisa na mama hakuna utata huyu ndiye Thomas" alisema Musa akiungwa mkono na majiraniwaliokuwa wamemzunguka wakati akitoa maelezo haya kwa mwandishi wa habari hizi.

Baada ya hapo kijana huyo alipelekwa kwa mganga wa tiba asiliaJuma Tabiho wa Kijijini hapo kwa lengo la kupatiwa matibabu kutokana na kijana huyo kuonekana hana utambuzi wa kawaida , hata hivyo jitihada za mganga huyo ziligonga mwamba kwani aliendelea kutokuwa katia utambuzi .

 Polisi Wilaya ya  Chato baada ya kupata taarifa hizo na kufika  kesho yake kijijini hapo na kuwakuta mamia ya wananchi wakiwa wamefurika nyumbani kwa mganga huyo wakiwa wanataka kwenda kufukua kaburi alikodaiwa kuzikwa kijana huyo.

Geita Yetu ikiwa eneo la tukio  ilimshuhudia mkuu wa Polisi wilayani Chato  Mrwa polisi Leonard Nyaoga akifanya kazi ya ziada kuwaelewesha wananchi hao taratibu za kufukua kaburi ambapo walimwelewa na kuwataka wasubiri taratibu za kisheria .

"Ndugu zangu wananchi hatuwezi kufukua kaburi kienyeji maana kufanya hivyo tutakuwa tunafanya kosa la jinai mpaka kibali cha mahakama, na inabidi wazazi na mtoto huyu wakachukuliwe vipimo vya DNA ili ukweli halisi ujulikane maana watu wengine hufanana" alisema OCD Nyaoga
Mkuu huyo wa Polisi alilazimika kuondoka na kijana huyo,   wazazi wake baadhi ya majirani wanaomfahamu vyema kijana huyo pamoja na viongozi wa Kijiji hicho  hadi kituo kikuu cha Polisi Chato kwa mahojiano zaidi.

Jeshi la Polisi mkoani hapa limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi taarifa zaidi baada ya kufanya uchunguzi na taratibu nyingine za kisheria huku likiwataka wananchi kuwa watulivu na kuendelea na shughuli zao kama kawaida.


Picha na Geita yetu Blog

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa