Mwandishi wetu, Bukombe-Geita Yetu
MBUNGE wa jimbo la Bukombe Mkoani Geita,
Profesa Kulikoyela Kahigi amewahimiza wananchi kukabiliana na mabadiliko ya
tabia nchi kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za uhifadhi wa mazingira.
Profesa Kahigi ameyasema hayo vijiji vya
Ibambilo na Isemabuna jana wakati wa mwendelezo wa ziara zake vijijini
kuhamasisha maendeleo kwa wananchi na kuelimisha wafahamu jinsi ya kukabiliana
na mabadiliko
hayo ya tabia nchi.
Amesema kutokana na mabadiriko ya hali ya hewa
hasa ukame inayolikabili taifa ni vyema wananchi kuanza kulima mazao ya alizeti
na muhogo kwa kuwa mazao hayo yanastahimili ukame na kwamba yanaweza kumkomboa
mkulima wa tanzania hasa wa jimbo la Bukombe.
Prof Kahigi asema kuwa mbali na mazao hayo ya
muhogo na alizeti kustahimili ukame lakini pia soko lake ni la uhakika na lenye
faida kubwa.
Mbunge huyo amewaasa wakulima kuwa sasa inawapasa wachukue hatua ili kukabiliana
na mabadiliko haya ya tabia nchi na kuachana na tabia ya kulima mazao ambayo
yamekuwa yakiwapa usumbufu kama vile zao la Pamba ambalo bei yake haina uhakika
na wamelima miaka mingi bila ya kuona mafanikio.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment