Na
Faida Muyomba, Geita
MBUNGE wa zamani wa jimbo la Nyang'hwale mkoani Geita,Bw. James
Msalika,ameibuka kidedea katika nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu
ya Chama cha Mapinduzi (nec)Taifa kupitia wilaya mpya ya Nyangh'wale,
baada ya kuwashinda wapinzani wake watatu.
Bw.Msalika aliyekuwa mbunge kwa muda wa miaka 12 aliashindwa kugombea ubunge,
baada ya kuangushwa na mbunge wa sasa wa jimbo hilo Bw.Hussein Amari wakati wa
kura za maoni ndani ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Katika uchaguzi huo uliofanyika jana katika ukumbi wa shule ya sekondari mjini
mjini Geita,Bw.Msalika alipata kura 503 kati ya kura 585 zilizopigwa na wajumbe
wa mkutano mkuu huo wa uchaguzi.
Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni mjumbe wa kamati ya siasa Mkoani
Mwanza,Bw.Kambandu Samweli aliwatangaza wagombea wengine katika nafasi hiyo
kuwa ni dkt.Peter Mwinginga aliyepata kura 57 na Bw. Jacob Nyanda ambaye pia ni
diwani wa kata ya Nyijundu kura tisa.
Kwa upande wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama hicho wilayani humo,msimamizi huyo
alimtangaza Bw.Adam Masudi Mtore kushinda kiti hicho kwa kupata kura 325,huku
wapinzani wake Bw. Mayunga Magiri (235) na Sostheness Ngusa akipata kura 25
Wajumbe watano wa mkutano mkuu wa CCM Taifa waliochaguliwa ni. Bi Helena
Shija,Bi .Agatha Marugumba,Bi .Veronika Makonge,Dkt Leonard Mugema na Donald
Kabosolo huku Said Lufunga Madoshi akichaguliwa kuwa Katibu wa itikadi na
Uenezi wilayani humo ambapo Bw. Richard Glani alichaguliwa nafasi ya
Katibu wa uchumi Wilaya.
Chanzo: Majira
0 comments:
Post a Comment