Ester Sumira, Geita
MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato,mkoani Geita wamemtaka Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Charles Maisha kueleza lilipouzwa gari jipya la halamashauri lililonunuliwa na Serikali kwa zaidi ya Sh200 milioni.
Wakizungumza kwenye kikao cha baraza jana, madiwani hao walikuja juu muda mfupi baada ya mwenyekiti huyo kufungua kikao.
Diwani wa Kata ya Mganza, Marco Maduka (Chadema) alikuwa wa kwanza kuomba mwongozo wa kanuni,kisha kutaka baraza hilo kupewa taarifa kuhusulilipo gari hilo ambalo ni mali ya halmashauri.
Gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser V8 ambalo lilikuwa maalumu kwa matumizi ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo,lilifanya kazi kwa miezi mitatu kisha ikadaiwa limeharibika injini na kupelekwa moja ya gereji za kutengeneza magari Mwanza.
Baadaye inadaiwa madiwani hao walipata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba, gari hilo lilihujumiwa na baadhi ya watumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo, kwa kuondoa injini yake na kuiuza kisha kuweka nyingine.
Kufuatia hali hiyo, madiwani hao walikuja juu na kumtaka aliyekuwa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, kabla ya kuvuliwa madaraka na kuhamishiwa sehemu nyingine,kurejesha gari hilo hasa baada ya kudai kubaini kuwa lilikuwa limepelekwa kwenye gereji ya ndugu yake.
Suala hilo liliwahi kufikishwa kwa Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Agrey Mwanri alipotembeleahalmashauri hiyo mwishoni mwa mwaka jana.
Mwanri alimtaka mkurugenzi huyo kutoa maelezo juu ya tuhuma hizo na kwamba, alikiri gari hilo kuharibika injini na kupelekwa Mwanza kwa matengenezo.
Diwani wa Kata ya Buseresere, Chrispine Kagoma alisema taarifa za uhakika ambazo madiwani wamezipata ni kwamba,Wakala wa Ufundi na Umeme (Tamesa) wamekataa kulitengeneza gari hilo kwa vile, vifaa vingi ikiwamo injini yake vimenyofolewa.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Ilemela, Ismael Luge alisema hawapo tayari kuona ufisadi mkubwa kama huo unaendelea kufanyika kwenye halmashauri hiyo, huku wao wawakilishi wa wananchi wapo na kumtaka mwenyekiti huyo kurejesha gari hilo hata kama ni bovu.
Akijibu hoja hizo, Maisha alisema suala hilo linashughulikiwa na taarifa zake tayari zipo na kuamua kuufunga mjadala huo, hali ambayo ilizusha manung’uniko kutoka kwa madiwani.
Miezi minane imepita tangu Waziri Mwanriaagize uongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo kurejesha gari hilo,lakini hadi sasa halijarejeshwa na hakuna sahihi ambazo zimetolewa kwa madiwani hao.
Chatoni miongoni mwa halmashauri zilizokumbwa na kashfa mbalimbali ikiwamo ubadhirifu wa zaidi ya Sh1.3 bilioniza pembejeo za wakulima,hali iliyopelekea Serikali kuwawajibisha mkurugenzi kwa kumvua madaraka, huku maofisa wengine waandamizi wakifikishwa mahakamani.
Chanzo: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment