Home » » VIONGOZI GEITA WAPEWA MBINU ZA KUDHIBITI WAHAMIAJI HARAMU

VIONGOZI GEITA WAPEWA MBINU ZA KUDHIBITI WAHAMIAJI HARAMU

Mwandishi wetu, Geita yetu
Idara ya Uhamiaji Mkoani Geita imeanza, kuendesha mafunzo ya kudhibiti wahamiaji haramu kwa viongozi wa kata mbili za Bugulula na Kagu mkoani humo.
Hadi Novemba mwaka jana, Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mwanza ambayo kiutawala bado inaulea mkoa wa Geita tayari ilikuwa imewatia mbaroni wahamiaji haramu 123 kutoka Burundi na Rwanda ambao wamekuwa wakiingia mkoa mpya wa Geita kwa ajili ya kilimo cha Nanasi na Mifugo.
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Omari Mselemu anasema suala la uhamiaji haramu lipodhibitiwa na viongozi wa vijiji, ipo hatari ya kuandikishwa na kupewa vitambulisho vya uraia kwa wahamiaji haramu
Amesema Wahamiaji Haramu wasipo dhibitiwa kuna hatari ya kupata viongozi wa ngazi mbalimbali wasio na uraia halali wa Tanzania.
Kwa upande wake kaimu afisa Uhamiaji mkoa mpya wa Geita Charles Washima sheria na kanuni za uhamiaji nchini zinazuia kumtunza muhamiaji haramu na wanaotenda kosa hilo wanatenda kosa la jinai
Mkuu wa wilaya ya Geita aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa kufungua mafunzo hayo Manzie Mangochie  anasema ni vyema wananchi wakafahamu kuwa ongezeko hilo la wahamiaji haramu nchini linaweza kusababisha matatizo kadhaa, ikiwemo kuhatarisha usalama wa nchi, pamoja na ongezeko la vitendo vya makosa ya jinai, kama vile ujambazi.
Mangochie anasema maeneo mengi ya Geita yamekuwa yakivutia wahamiaji,lakini yapi madhara makubwa ya kuwahifadhi wahamiaji haramu.
Mkoa wa Mwanza unaendesha mafunzo kwa vingozi wa vijiji na kata kujua madhara na hatimaye kudhibiti uhamiaji haramu
Blogzamikoa

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa