Home » » DC Geita aamuru shule ya sekondari ivunjwe

DC Geita aamuru shule ya sekondari ivunjwe

Na David Azaria, Geita-Geita Yetu 
Mkuu wa wilaya ya Geita katika mkoa mpya wa Geita, Manzie Mangochie ameanza kazi kwa kusitisha ujenzi wa sekondari ya kata ya Lubanga wilayani hapa kwa kile alichodai eneo hilo lilistahili kujengwa Hotel ya kitalii na si shule. 
Mkuu huyo wa wilaya alisitisha ujenzi huo jana (juzi) alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye kata hiyo ikiwemo shule hiyo iliyojengwa kwa nguvu za wananchi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya serikali za mitaa yaliyofanyika kiwilaya katika kijiji cha Lubanga wilayani geita. 
Hata hivyo akiwa eneo ilipojengwa shule hiyo alipigwa na butwaa kuona imejengwa juu ya mlima wenye mawe mengi na baada ya kuhoji eneo la wanafunzi watakapojipanga eneo la ukaguzi na utakapowekwa uwanja wa  michezo wa shule aliamua kusitisha ujenzi huo mara moja baada ya kukosa majibu ya kuridhisha kutoka kwa viongozi wa serikali wa eneo hilo. 
“Huwezi kusema eti wewe ni mgeni na umekuta ujenzi wa shule umeshafanyika utetezi wenu haufai kutolewa na viongozi walio makini naomba mtafute eneo lingine la kujenga shule na si hapa kwani hakuna hata eneo la wanafunzi kupanga paredi”alisema Mangochie na kuongeza. 
“sifa ya kwanza ya eneo la kujenga shule liwe la wazi na tunajua shughuli za binadamu zinaongezeka lakini hatupaswi kuchukua maamuzi ya kutaka kukomoana na kupoteza nguvu za wananchi bure kwani hili eneo linafaa kujengwa hoteli ya kitalii” 
Aliongeza“hebu mnieleze hapa viwanja vya michezo vitakuwa wapi wanafunzi watajipanga wapi wakati wa ukaguzi hivi kweli tunao umasikini wa ardhi hadi shule ijengwe kilimani naomba ujenzi huu usitishwe mara moja na muwaone wataalamu waje wawatafutie eneo lingine la wazi ambapo kutakuwa na eneo la kuweka uwanja wa michezo, pamoja na sehemu ya wanafunzi kujipanga kwa ukaguzi hapa hapafai”. 
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya alipiga marufuku viongozi wa wananchi kufanya maamuzi ya kuanzisha miradi ya maendeleo pasipo kushirikisha wataalamu ambao wameajiriwa kwa kazi hiyo na kulipwa mishahara minono. 
“Sitaki kuona wala kusikia viongozi wa wananchi mnafanya mambo kienyeji bila kushirikisha wataalamu ambao wameajiriwa kwa kazi hiyo na wanalipwa mishara minono hata hapa mngekuwa mmeshirikisha wataalamu hata hili la kujenga shule milimani lisingejitokeza”alisema 
Awali katika utetezi wao ofisa mtendaji wa kata ya Lubanga Sekile Mhangwa,Diwani Nyanda Brashi,Mwenyekiti wa kijiji Joseph Chagula na mwenyekiti kamati ya shule walidai wakati wa ujenzi huo ukifanyika walikuwa hawajateuliwa kushika nyadhifa walizonazo katika kata hiyo utetezi ambao ulitupiliwa mbali  na mkuu huyo wa wilaya kwa madai kuwa hauna mashiko. 
Aidha shule hiyo imefikia kiwango cha ujenzi wa madarasa matatu huku madarasa mengine yakiwa kwenye msingi pamoja na nyumba mbili za walimu na iwapo itavunjwa itakuwa imerudisha nyuma juhudi za wananchi za kutaka shule ianze kutumika mapema mwakani. 

0 comments:

Post a Comment

Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa