Halmashauri ya wilaya ya Geita imefanikiwa kugawa vyandarua vyenye
viuwatilifu 131,445 kwa uwiano wa chandarua kimoja kwa watu wawili kwa
jumla ya kaya 467,609 katika harakati za kutokomeza ugonjwa wa malaria
ambao bado ni tishio kwa eneo la kanda ya ziwa.
Akiongea wakati wa kikao cha
kutathimini hali ya malaria wilayani hapa kaimu mratibu wa malaria
wilaya ya Geita ndugu Fredy Mwaipaja amesema Maambukizi ya malaria
yamepungua kutoka asilimia 16.3% mwaka 2016 hadi 15.1% mwaka 2017 kwa wagonjwa 112,134 sawa na asilimia 36.5% kati ya wagonjwa 310,251 waliofika katika zahanati na vituo vya afya ambao ni wagonjwa wa nje maarufu kama OPD .
Utafiti wa malaria uliofanyika mwezi Oktoba, 2017 katika shule 5 za Msingi Halmashauri ya wilaya Geita unaonyesha wanafunzi 396 kati ya 674 sawa na asilimia 58.8%
ya wanafunzi waliopimwa waligundulika na vimelea vya Malaria hali
iliyopelekea Halmashauri kuja na mkakati mwingine wa kuhakikisha
vyandarua vyenye viwatilifu vinagawiwa shuleni na pia watoto
wanafundishwa mbinu mbalimbali za kupambana na Malaria.
Mwaipaja ameeleza kiwango cha upimaji wa malaria kimeongezeka kutoka asilimia 91.8% mwaka 2016 hadi asilimia 98.8% mwaka 2017 na watu waliogundulika wana malaria walipatiwa tiba.
Akilezea Sababu zinazochochea
maambukizi ya malaria katika jamii ni pamoja na tabia ya jamii kuchelewa
kufika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwa ajili ya utambuzi na
kupata tiba ya malaria, Kutumia dawa bila kupima, kutokamilisha dozi
kwa wagonjwa wa malaria, Matumizi yasiyo rasmi ya vyandarua kwa shughuli
zisizokusudiwa pamoja na Kugomea shughuli za unyunyiziaji wa dawa ya
ukoko majumbani”.
“Katika kuhakikisha Malaria
inaondoka kabisa Geita kwa sasa tunatoa elimu kwa jamii na tunahakikisha
matumizi salama na sahihi ya vyandarua yanatelekezwa na ndio maana
tumeamua kugawa vyandarua hivyo kwenye ngazi za shule za msingi kama
njia mojawapo ya kuzuia malaria” Ameongeza Mwaipaja.
Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi
wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita baina ya Wataalam kutoka Halmashauri ya
wilaya ya Geita pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali ya “Tanzania
Communication and Development Center”(TCDC),Pamoja na New Light Children
Organisation (NELICO) kwa lengo la kutathimini hali ya Ugonjwa wa
Malaria wilayani hapa.
0 comments:
Post a Comment