Home » » Geita DC yapitisha Bilioni 77.6 Mwaka wa Fedha 2018/2019

Geita DC yapitisha Bilioni 77.6 Mwaka wa Fedha 2018/2019

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 

Na Bathromeo C Chilwa
Afisa Habari Geita DC

Baraza la madiwani Halmashauri ya wilaya ya Geita limepitisha makadirio ya bajeti ya matumizi ya mwaka wa fedha 2018/2019 kiasi cha shilingi bilioni 77,673,234,821. Ikiwa ni ongezeko la shilingi bilioni 1,173,780,082.13 sawa na asilimia 1.5 % kutoka katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 kiasi cha shilingi bilioni 76,499,454,738.87, iliyotengwa .
Katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita kikao cha baraza  la madiwani  kiliongozwa na Mheshimiwa Hadija Said Makamu mwenyekiti wa Baraza hilo na kuhudhuriwa na Mbunge wa jimbo la Busanda Mheshimiwa Lolensia Bukwimba, Waheshimiwa Madiwani, Wataalam wa Halmashauri, Viongozi wa vyama vya siasa na wadau wengine wa maendeleo kutoka wilayani hapa.
Katika bajeti hiyo shilingi bilioni 18,040,010,550/=  ambazo ni fedha za ruzuku zitatumika kutekeleza miradi ya maendeleo, Shilingi bilioni 2,440,501,771/= ni fedha za ruzuku zitakazotumika kwa matumizi ya kawaida (OC), Shilingi bilioni 53,607,008,000/= zitatumika kulipa mishahara, shilingi bilioni 3,585,714,500/=  ni makusanyo ya ndani, shilingi bilioni 1,297,941,800/= ni matumizi ya kawaida ya mapato ya ndani (OS) na Shilingi bilioni 2,084,412,700/= zitatumika kutekeleza miradi ya maendeleo, shilingi milioni 203,360,000/= ni matumizi ya mapato mengine ambayo ni (CHF,NHIF/User fee) na shilingi bilioni 1.5 zitakuwa ni nguvu za wananchi kuchangia miradi ya maendeleo.
Sambamba na hilo Halmashauri  imeainisha chanzo kipya cha mapato ambacho ni kituo cha redio cha rubondo kinachotarajiwa  kuanza kazi hivi karibuni kukasimiwa katika bajeti na kukadiriwa kuingiza kiasi cha shilingi milioni 250.
Bajeti hii  ina matarajio makubwa ya kuboresha huduma za jamii kupitia sekta za Elimu, Afya, Maji,Ardhi na Mifugo, Pia Kuboresha miundombinu ya ufundishaji na kufundishia mashuleni kwa kujenga shule za elimu ya juu(A’Level), Hosteli za wasichana, Vyumba vya madarasa,Nyumba za walimu, Maabara na kutoa Motisha kwa walimu kwa lengo la kuongeza ufanisi.
Source www.geitadc.go.tz

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa